- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani Yang’ara Solya Sekondari
Manyoni, Oktoba 11, 2025 – Shule ya Sekondari ya Wasichana Solya imeandikisha historia kwa kuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, yaliyojaa hamasa, elimu, ushawishi na midahalo yenye lengo la kuinua hadhi ya mtoto wa kike katika jamii.
Mgeni rasmi alikuwa RAS mstaafu wa Mkoa wa Singida, Bi. Dorothy Mwaluko, ambaye aliwasihi watoto wa kike kujiamini, kusoma kwa bidii na kutambua nafasi yao kama viongozi wa kesho. “Mtoto wa kike si wa kumhurumia, bali wa kumuandaa kuwa kiongozi imara wa kesho,” alieleza kwa msisitizo.
Aliambatana na Bi. Lucy Deu, Mganga Mfawidhi Wilaya ya Manyoni, ambaye alihimiza umuhimu wa afya ya mtoto wa kike na kuwatia moyo wasichana kuwa na maono makubwa. “Mkijitahidi kusoma, mtakuwa viongozi bora mnaomwakilisha Mungu katika jamii,” alisema.
Aidha, mwanasiasa na mtetezi wa haki za wanawake na watoto Bi. Tatu Nasoro aliwahamasisha wanafunzi kujitambua, kusimamia ndoto zao na kutokubali kukatishwa tamaa.
@drmashinjivincent @anastaziatutuba @singidars @halimadendego
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.