- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
BARAZA LA Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, limeshauri usimamizi mzuri wa fedha za miradi zilizotolewa na serikali kwa Halmashauri hiyo. Aidha Baraza limesisitiza utekelezaji wa miradi hiyo kukamilika kwa wakati na ubora uendane na thamani ya fedha iliyotolewa.
Baraza la Madiwani, lililoongozwa na Mwenyekiti Mh Jummane Mlagaza lilikaa tarehe 23 Septemba2022. Baraza pia liliishukuru Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani kwa kutoa pesa za miradi mbalimbali kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Fedha zilizotolewa ni kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa kituo cha afya kwenye kata ya Sanza, Shule ya sekondari ya Wasichana Solya,ujenzi wa jengo la OPD na miradi mingine inayotarajiwa kutekelezwa.
Baraza la madiwani lililofanyika tarehe 23 Septemba 2022 lililoongozwa na Mwenyekiti Mh Jumanne Mlagaza katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni lilihudhuriwa na Katibu Tawala Wilaya, Mh mbunge Dkt Pius Chaya, Mkurugenzi wa halmashauri Melkizedeck O. Humbe, Makamu mwenyekiti Mh Haruna Thomas, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Taasisi mbalimbali, Maafisa Tarafa,Wakuu wa Division na Vitengo na waandishi wa habari
.Akizungumza kwenye Baraza hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manyoni, Melkizedeck Humbe, alisema,
“Tumepokea changamoto mbalimbali, tutazifanyia kazi. Tunaenda kuongeza mashine za POS kwaajili ya kukusanyia mapato na kila Mtendaji wa Kijiji atakua na mashine yake ili kuongeza na kuboresha ukusanyaji wa mapato katika halmashauri yetu,”
Alieleza kwamba, hiyo itasaidia kutekeleza miradi ya maendeleo mbalimbali na kuisimamia. Alisisitiza kwamba kama jambo lipo kwenye bajeti ni vema kulitekeleza na kuepuka kuweka matumizi mapya ya fedha. “Naomba tushirikiane wote katika hili.Nawapongeza waheshimiwa Madiwani kwa kushiriki vema katika majukumu yao,”
Waheshimiwa Madiwani wakiendelea kufatilia majadiliano ndani ya Baraza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni akizungumza kwenye Baraza
Aidha baraza pia lilifanya Uchaguzi wa Makamu mwenyekiti ambapo Chama cha Mapindizi kiliwasilisha Jina la Mh Haruna Thomas kama mgombea,Wajumbe halali 26 walipiga kura na Mh Haruna alishinda kwa kupata kura 24 ambazo ni sawa na asilimia 92.
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea baada ya wajumbe kupiga kura
Mh Mwenyekiti wa Baraza pia, aliziasa kamati zote kwa nafasi zao kusimamia na kutekeleza majukumu yao ili kusaidia halmashauri ya Manyoni . Chama Cha Mapinduzi kupitia wananchi kimetuamini ili kusimamia maendeleo kwa misingi ya sheria na taratibu za nchi, Kwa pamoja tunaweza kuleta maendeleo ndani ya Halmashauri yetu
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.