- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni leo tarehe 26/02/2019 limepitisha makisio ya mpango na bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 kiasi cha Tsh. 26,203,499,412/= Kati ya fedha hizo Tshs. 1,450,783,500/= ni ruzuku ya miradi ya maendeleo na wahisani, Tshs 1,068,707,056 ni ruzuku ya matumizi ya kawaida, Tshs. 20,788,360,000/= mishahara, na Tshs 2,677,435,396 ni mapato ya ndani.
Aidha Halmashauri imejiwekea mikakati mbalimbali ili kuhakikisha ukusanyaji wa mapato ya vyanzo vya ndani unaimarika na kuwa wa ufanisi zaidi. Mikakati hiyo ni pamoja na Kuendeleza ujenzi wa stendi ya Mabasi na eneo la kupaki magari makubwa na uboreshaji wa masuala mbalimbali ya Kilimo ikiwemo kilimo cha korosho na ukarabati wa skimu mbalimbali za umwagiliaji. Vilevile katika huduma za jamii bajeti hiyo ya 2019/2010 itawezesha uboreshaji wa majengo ya kutolea huduma za afya na elimu, pamoja na mikopo ya wanawake na vikundi vya watu wenye ulemavu.
Vipaumbele vya miradi ya maendeleo vya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 vimejikita katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Ujenzi, Utawala, Maendeleo ya Jamii, Fedha na biashara, Uvuvi, Mifugo na Sekta ya Kilimo.
Katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya wilaya ya Manyoni iliidhinishiwa kukusanya kiasi cha jumla ya Tshs 23,315,636,767/=. Kati ya kiasi hiki Tsh 17,767,620,785/= zinatumika kwa ajili ya mishahara, Tsh 697,784,747/= kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Tsh 2,258,809,990/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Mpaka kufikia Desemba 2018 upande wa maeneo yasiyo ya ruzuku, halmashauri ilikuwa imekusanya jumla ya kiasi cha Tsh 871,723,854/= kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya halmashauri sawa na asilimia 32 ya makisio ya 2018/2019.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.