- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kaimu mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Dr. Francis Alfred leo Julai 20, 2019 amekabidhi pikipiki 4 katika halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa ajili ya kuwawezesha maafisa ugani waliopo Halmashauri ya Manyoni kutembelea miradi mbalimbali ya Korosho ukiwemo mradi mkubwa wa shamba la Korosho la Mkwese – Masigati lenye ukubwa wa Takribani ekari 12000.
Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Mkurugenzi wa bodi ya Korosho Tanzania alisema, kazi kubwa ya Bodi ni Kusimamia, Kuhamasisha na Kuwezesha ukuaji wa zao la Korosho. Hivyo wao kama Bodi ya korosho kupitia Wizara ya kilimo wameamua kuleta Pikipiki 4 kati ya 10 ambazo wamepanga kuzileta Manyoni kwa ajili ya Usimamizi wa uzalishaji wa zao la korosho. Vilevile ameushukuru Uongozi wa mkoa na Wilaya kuanzia kwa Mkuu wa mkoa wa Singida Mh Dr. Rehema nchimbi na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh. Rahabu Solomon kwa juhudi zao za kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kilimo.
Akizungumza katika kutoa Shukrani baada ya kuzipokea, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndugu Charlles Fussi aliishukuru Wizara ya Kilimo kupitia bodi ya korosho kwa kuwapa pikipiki hizo na kuahidi kuzitumia katika kukuza na kuimarisha uzalishaji wa zao la korosho katika Mradi na kwa wakulima waliolima nje ya mradi, lengo ni kuhakikisha halmashauri nzima inasimamiwa vyema na maafisa ugani ili kukuza uzalishaji wa zao la korosho ambalo litapelekea wananchi kuwa na zao la kudumu la Biashara hivyo kuwapunguzia adha ya kuuza mazao ya chakula.
Nae Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mh. Daniel Mtuka aliishukuru Wizara ya Kilimo kwa uamuzi walioufanya wa kufungua Ofisi ya Bodi ya Korosho kanda yaka kati katika Mji wa Manyoni ambapo imewapa hamasa wakulima kuendelea kuthamini zao la korosho na hivyo wengi wanaanza kuamka na kushiriki katika kilimo cha korosho kuanzia Majumbani kwao.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.