- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakulima wa korosho wilayani Manyoni wametakiwa kuzingatia mafunzo na maelekezo yote wanayopatiwa na watalaamu wa kilimo ili kuweza kuimarisha na kuboresha kilimo cha korosho kuwa bora na chenye tija.
Hayo yamesemwa tarehe 18/11/2020 na BODI ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI) walipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni katika ziara yao ya kuangalia mafanikio ya kilimo cha Korosho ikiwa ni moja ya maagizo yanayotekelezwa na Taasisi hiyo kupitia Taasisi ya Utafiti wa kilimo cha Korosho Naliendele.
Akizungumza kwa nyakati tofauti Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Dkt Yohana Budeba ametoa wito kwa watafiti wake sambamba na wadau wa taasisi hiyo kuhakikisha wanaongeza kasi zaidi katika kuleta mapinduzi ya kilimo, aliwataka watafiti na wadau wengine wa kilimo kuunga mkono juhudi za serikali ili kuchagiza kasi ya mabadiliko hayo, sanjari na kusukuma ukuaji wa uchumi.
“Kwa mujibu wa Rais Magufuli serikali imedhamiria kuongeza juhudi ili kubadilisha kilimo cha Tanzania kuwa cha kibiashara. Hivyo ni jukumu letu watafiti na wakulima kwenda pamoja na dhamiri hiyo njema ili kuongeza tija” alisema Budeba
Alisema katika kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo na maelekezo ya serikali, Bodi yake imefarijika sana kuona utekelezwaji wa maagizo ya bodi hiyo inayoundwa nawajumbe 12 kutoka taasisi na wadau mbalimbali,
Moja ya agizo lilikuwa ni kuitaka TARI kufanya tafiti yenye lengo la kupanua wigo wa kilimo cha zao la korosho kutoka mikoa 5 iliyokuwa ikilima zao hilo, jambo ambalo nalo limetekelezwa ipasavyo kwa taasisi hiyo mpaka sasa kufanikisha kwa tija uanzishwaji wa kilimo cha zao hilo kwa mikoa takribani 20 ikiwemo Singida, ambayo alipongeza kwa kuendelea kufanya vizuri hususan kupitia shamba lake la Masigati, Manyoni lenye takribani ekari elfu 22 zinazolimwa zao hilo kwa tija na mafanikio makubwa
Dr Budeba pia aliwapongeza mkuu wa wilaya ya Manyoni Mh Rahabu Mwagisa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Manyoni ndugu Charles Fussi pamoja na watendaji wanaosimamia kilimo kwa kuonesha moyo wa kusimamia wakulima na kukubali kulima zao la korosho ambapo kwa msimu wa 2020/2021 wakulima wanatarajiwa kuvuna mazao na kuingia kwenye soko.
Lakini pia amepongeza mkoa wa Singida hususani wilaya ya Manyoni kwa kubuni zao la kimkakati na kuteua baadhi ya maeneo ili kulima korosho
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TARI nchini, Dkt Geofrey Mkamilo, alisema hitaji la Taasisi hiyo kwa sasa ni kuona uzalishaji wa teknolojia zake, ubunifu na mbinu bora za kilimo zinakwenda sambamba na ukuaji wa viwanda-huku taasisi ikiahidi kuongeza juhudi katika kuhakikisha kiwango cha asilimia 60 za malighafi ya kilimo kwenye viwanda vya ndani na zaidi ya hapo inafikiwa ipasavyo.
Alisema pamoja na mambo mengine, shabaha iliyopo mbali ya kupanua wigo wa huduma za kiugani kwa kushirikiana na wadau, taasisi imejipanga kuongeza uzalishaji wa mbegu za korosho ili kukidhi mahitaji ya mikoa yote 20 inayolima zao hilo, na stratejia iliyopo ni kuzalisha kutoka wastani wa tani takribani laki 3 zinazozalishwa kwa sasa kufikia tani milioni 1 ifikapo 2024.
“Maono ya Rais Magufuli ni kuona tija inaongezeka zaidi kupitia hasa mazao haya ya kimkakati likiwemo zao la korosho. Na katika hili tumejipanga vizuri kuhakikisha tunakwenda kuzalisha mabilionea wa kutosha kupitia takribani mazao yote 85 ikiwemo korosho tunayoshughulika nayo, lengo ni kumtoa mkulima kutoka kwenye kilimo cha kujikimu kwenda kwenye kile cha kibiashara” alisema Mkamilo.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.