- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo tarehe 27 febuari amefanya ziara yake katika Wilaya ya Manyoni kwa lengo la kuhuisha chama na kufatilia utekelezaji wa Ilani ya Chama, ambapo moja ya mradi aliotembelea ni Ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Solya.
Chongolo ameeleza namna alivoridhishwa na Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana kuanzia ubora wa Majengo mpaka hatua ujenzi huo ulipofikia.
“Kwa namna nilivojionea hapa ujenzi huu nimeridhishwa nao, Majengo yanaonekana kabisa ni imara na kwa taarifa mliyosoma hapo hakuna fedha imepotea katika ujenzi huu”
Niwashukuru kwa namna viongozi wote kuanzia Mkuu wa Mkoa, RAS,Mkuu wa Wilaya’ Mkurugenzi na Wataalamu wako kwa namna mlivojitoa kusimamia mradi huu wa zaidi ya Bilioni tatu (3) hakika kazi ni nzuri. Kwa wakati mwingine niwashauri kuanza kujenga majengo muhimu kwanza kulingana na fedha iliyopo ili jamii ianze kuapata huduma kwanza kabla ya kusubiri fedha za kumalizia majengo mengine. Alisisitiza Chongolo
Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba alitumia fursa hiyo kumuomba Katibu Mkuu kupata kiasi cha shilingi Bilioni Moja iliyobaki katika ujenzi huo wa shule ya wasichana solya uliofikia hatua mbalimbali katika ujenzi wake.
“Ujenzi huu wa shule ya sekondari ya wasichana Solya tulipewa Bilioni nne (4) ili kuhakikisha majengo yote yanakamilika lakini mpaka sasa tulizozipokea ni Bilioni tatu (3) hivyo Katibu mkuu tuanaomba tupatiwe na hiyo Bilioni moja (1) iliyobaki ili tukamilishe majengo yote na mwakani shule hii ifunguliwe na watoto waanze kusoma”.
MATUKIO KWA PICHA.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.