- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
CRDB Bank Yachangia Madawati Solya Sekondari Viti 50 na meza 50, Ded Tutuba Atoa Shukrani na Wito wa Kuhifadhi Mazingira
Katika hafla yenye mvuto wa kipekee iliyofanyika katika Shule ya Wasichana ya Sekondari ya Solya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Bi. Anastazia Tutuba, ameipongeza na kuishukuru kwa dhati Benki ya CRDB kwa mchango wao wa madawati kwa shule hiyo.
Akizungumza Bi. Anastazia Tutuba mgeni rasmi, alieleza kuwa mchango huo ni uthibitisho wa namna taasisi binafsi zinavyoweza kushiriki moja kwa moja katika kuinua sekta ya elimu nchini. Alisisitiza kuwa uwekezaji katika elimu ya mtoto wa kike ni msingi wa maendeleo ya jamii nzima.
Katika hotuba yake, alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wanafunzi kupinga vikali ndoa za utotoni na kujikita katika masomo ili kufikia ndoto zao. Aidha, alitoa wito kwa CRDB Bank kupitia mfuko wao wa kuboresha mazingira, kurejea katika shule hiyo kwa ajili ya kupanda miti, kama sehemu ya kuimarisha mazingira ya kujifunzia.
“Tunathamini sana sapoti yenu. Mmeonesha kuwa elimu si jukumu la serikali pekee, bali la jamii nzima. Tushirikiane kuiendeleza Manyoni,” alihitimisha Bi. Tutuba kwa msisitizo na shukrani.
@anastaziatutuba @drmashinjivincent @halimadendego @crdbbankfoundation @singidars
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.