- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Mwagisa ametoa wito huu jana tarehe 17 januari 2023 baada ya kutembelea shule mbalimbali za msingi na sekondari akiambatana na Kamati ya siasa ya Wilaya ilipokua ikifatilia Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Ameona hali ya mwenendo mahudhurio ya wanafunzi wa kidato cha kwa kwanza kurepoti katika shule walizopangiwa, ambapo hadi sasa idadi ya wanafunzi walioripoti hairidhishi ikilinganisha na matarajio.
“ Wito wangu Nataka wazazi walete wanafunzi kuripoti shule walizopangiwa kidato cha kwanza haraka iwezekanavyo kwakua Elimu ni bure na huku wakiendelea kukamilisha mahitaji mengine, Walimu wapokeeni wanafunzi hata kama bado hana sare za shule watakamilisha taratibu. Nimepita katika shule chache ambazo tumeona mahudhurio ya wanafunzi kuripoti sio mazuri , nimepita Sasilo, saranda imeonesha hali halisi.
Ifikapo tarehe 30 januari wanafunzi wote wawe wamesharipoti shule walizopangiwa kwa ambao hawataleta wanafunzi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Watendaji na viongozi wengibne wa serikali naomba mlisimamie hili kuhakikisha watotot wanaripoti shule wote ifikapo tarehe 30 na muwabaini ambao watakua hawajaripoti kwa hatua Zaidi za kisheria”. Amesisitiza Mhe. Mwagisa.
Aidha kutokana na hali hiyo Mhe. Mwagisa aliwataka wazazi kutambua wajibu wao na umuhimu wa Elimu kwa Watoto, Hivyo basi wahakikishe Watoto wanaripoti shuleni mapema na kwa muda uliopangwa.
Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutenga fedha kwaajili ya kuboresha miundombinu ya vyumba vya madarasa nchi nzima ili kuleta utoshelevu wa mazingira ya kujifunza na kujisomea kwa idadi ya wanafunzi waliopangiwa katika shule hizo hvyo ni wajibu wetu kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita kwa kuhakikisha Watoto wanafika shuleni mapema kwaajili ya kuanza masomo yao.
Sambamba na hilo Mhe. Mwagisa amewataka Wakuu wa Shule kwa kushirikiana na Kamati za Shule kuitisha mikutano ya mara kwa mara na wazazi wa wanafunzi ili kukumbushana wajibu na majukumu katika kutimiza haki za msingi za wanafunzi kupata elimu ikiwa ni pamoja na kutambua kuwa wanafunzi wanapaswa kuripoti shuleni mapema ili kuendana sawa na mihula ya shule na kuhakikisha wanfunzi wanasoma kuanzi siku ya kwanza aliyopaswa kuwepo shuleni.
“Kuna haja ya kuwepo mikutano ya wazazi ya mara kwa mara katika shule zetu hivyo niwaombe sana walimu mkishirikiana na kamati zenu za Shule kuandaa mikutano hii na kukumbushana juu ya wajibu wa mzazi na jamii inayomzunguka kwa ujumla ili kuhakikisha wanafunzi hawa wanapata elimu kikamilifu na kwa wakati sahihi, Moja ya wajibu wa wazazi kwa wanafunzi ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanaripoti shuleni siku ya kwanza wanapofungua shule ili waende sawa na muhula ulivyopangwa”
“Nitoe wito kwa Walimu kutoa elimu kwa wazazi kuhusu umuhimu wa elimu pamoja na malezi kwa Watoto kutokana na wazazi wengi kupuuzi umuhimu wa elimu kwasasa na kupelekea kuathiri mwenendo w a wanfunzi katika ufaulu. Pia amewaomba walimu kutoa elimu ya malezi kwa kushirikiana na wazazi kwasababu wanafunzi wengi kwa sasa wana changamoto ya malezi hali inayopelekea mporomoko mkubwa wa maadili na kuathiri ufaulu wa wanafunzi”
Ni Imani yangu kuwa viongozi mnakwenda kuyasimamia haya niliyoyasema hapa na kuhakikisha ifikapo tarehe 30 januari wanafunzi wote ambao ni matarajio yetu kwa mwaka 2023 wanaripoti shuleni kwa shule zote kwa kidato cha kwanza na darasa la kwanza na Awali. Serikali imeweka mpango bora wa elimu bure ili kuhakikisha Watoto wote wa jinsia zote wanapata elimu bora na kwa usawa.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.