- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
*DED MANYONI AKABIDHIWA KOMBE LA USHINDI WA TATU- DRAFTI KATIKA MASHINDANO YA SHIMISEMITA KITAIFA – TANGA*
*Manyoni, 01 Sept 2025*
Mkuu wa Kitengo cha Sanaa na Michezo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg. Abubakar Kisuda pamoja na Timu ya Kurugenzi Manyoni leo wamemkabidhi rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (DED) Bi. Anastazia Tutuba kombe la ushindi wa tatu katika mchezo wa Drafti, baada ya timu ya Manyoni kurejea kutoka kushiriki mashindano ya *SHIMISEMITA* ngazi ya Taifa yaliyofanyika jijini Tanga.
Tukio hilo limefanyika ofisini kwa Mkurugenzi huku kikosi cha timu ya michezo Manyoni kikishuhudia kwa furaha na fahari. Timu ya Kurugenzi Manyoni iliwakilisha Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni katika mashindano hayo, na kuibuka mshindi wa tatu Kitaifa katika mchezo wa Drafti, ikiwashinda wapinzani kutoka Halmashauri mbalimbali.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mkuu wa Kitengo cha Sanaa na Michezo alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri kwa usaidizi na usimamizi mzuri uliowezesha timu kufika mbali. Alieleza kuwa ushindi huo ni matokeo ya juhudi za pamoja, nidhamu ya wachezaji, na uwekezaji wa Halmashauri katika sekta ya michezo.
Kwa upande wake, Bi. Anastazia Tutuba Mkurugenzi wa Halmashauri aliipongeza timu kwa ushindi huo na kusema:
*"Ushindi huu si wa Drafti tu, bali ni ushindi wa nidhamu, kujituma, na uwakilishi mzuri wa Halmashauri ya Manyoni. Tutaendelea kuwekeza katika vipaji ili michezo iwe sehemu ya maendeleo yetu."*
Mbali na kombe, Mkurugenzi pia alipokea Cheti rasmi cha ushiriki kutoka kwa waandaaji wa SHIMISEMITA, kama kumbukumbu ya mchango wa Manyoni katika mashindano hayo.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.