- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Walimu wakuu , Maafisa elimu na Viongozi wa idara ya elimu msingi tarehe 11 Januari 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wamekaa kikao cha tathimini ya matokeo ya darasa la saba 2022 na kuweka Mikakati ya namna ya kuboresha ufundishaji ili kupandisha ufaulu.
Akizunguza katika kikao hicho Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Manyoni Mwl. Hamisi Milowe amesema; Matokeo sio mazuri sana tukilinganisha na matokeo ya Mock kwani yalitupa matumaini na muelekeo wa kufanya vizuri sana. Lengo la serikali na kila shule iwe na ufaulu wa 85% hivyo msipofikia lengo hili mnashusha wastani wa ufaulu kwa Halmashauri. Hivyo tuwe na mikakati mizuri ili tufikie lengo.
Matumizi ya vitabu vya mitihani, watahiniwa watumie vitabu hivi vya mitihani (PIRA) ili kuongeza na kukuza uelewa na pia vyakula mashuleni ni lazima tujitahidi kuhakikisha kuna vyakula shuleni ili kupunguza watoto kukaa muda mrefu bila kula na badala yake kuwaza chakula na sio masomo.Alisema Mwl. Milowe.
Muunde kamati ya Taaluma ya Kata ambayo kamati yake wajumbe wake ni Walimu wakuu wote,kamati hii ndio inapaswa kufatilia taaluma kwa shule zote ndani ya kata nzima. Na Kamati ya uthibiti ubora ndani ya shule kila jumatatu ikae kikao kuona maendeleo ya shule husika.
Mkakati mwingine ni pamoja na kuhakikisha tunapunguza au kuondoa kabisa utoro kwa kutoa motisha kwa wanafunzi na walimu wanaofanya vizuri shuleni, michezo shuleni, bendi na pia ziwepo sheria ambazo zitadhibiti utoro kwa kiasi kikubwa.
Mwl. Milowe alisema “ Tukamilishe miundombinu kwa wakati na miradi ilingane na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali. Maafisa Elimu na wakuu wa shule wakae kwenye maeneo yao ili kusimamia miradi shuleni. Pia wakuu wa shule msikumbatie miradi shirikisheni walimu wote waijue miradi ili inapotokea haupo basi kila mmoja aweze kuuelezea mradi. Kamati za usimamizi wa miradi ziundwe mapema ili inapokuja miradi uanze mara moja”.
Tuko nyuma sana kwenye suala la uandikishaji kwa wanafunzi wa Awali na darasa la kwanza hivyo naomba tujitahidi tuendelee kuandikisha ili tupige hatua kwani tupo nyuma sana, Samabamba na hilo tuendelee pia kupokea Watoto wenye mahitaji maalumu. Alisema Mwl. Milowe.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.