- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Salehe Mkwizu pamoja na baadhi ya Madiwani, Wenyeviti wa vijiji na wataalamu wa kilimo leo wametembelea mashamba ya korosho yaliyopo katika Kijiji cha Masigati katika Halmashauri ya Manyoni kuona kile ambacho kinafanyika ili kuweza kujifunza namna sahihi ya kufanikisha kilimo hicho kama kinavyofanya vizuri katika Mradi wa Mkwese – Masigati ambao unasimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Akizungumza na Afisa kilimo pamoja na Mwenyekiti wa wakulima wa korosho Wilaya ya Manyoni, kwa niaba ya Madiwani wote wa Wilaya ya Mwanga Mh Mkwizu amesema kuwa wamekuja kujifunza kutoka kwa wataalamu wa Manyoni kwani katika Wilaya ambazo korosho Ni zao la kimkakati na Wilaya ya Mwanga nayo pia Ni mojawapo hivyo wamekuja kuona Ni jinsi gani Manyoni inafanikiwa katika uzalishaji wa zao hilo.
Mh Mkwizu amesema kuwa wamefurahishwa sana na kwamba Sasa nao wanaenda kuanza kutumia hayo waliyoyapata kutoka kwa wataalamu ili na wao waweze kukazania kilimo hicho Cha korosho Wilayani humo.
Aidha Mh Mkwizu amesema kuwa Wilaya ya Mwanga Ni Wilaya yenye kufanana Kihali ya hewa na Manyoni hivyo Kuna tija ya kuendelea kujifunza mengi kutoka Manyoni na kwamba Kuna tija pia ya kuungana kwa pamoja ili siku Moja na wao pia waje wawe Kama Manyoni.
"Niseme tu kuwa kwakweli tumefurahishwa Sana na jinsi ambavyo mmetupokea na kutupatia huu utalaamu na kwamba tunawaahidi tunakwenda kuanza Sasa na ikifika wakati tutawaita mje muone Yale ambayo mmetufundisha jinsi tunavyoyatekeleza lakini pia niombe msituchoke tutaendelea kuhitaji ushauri wenu wa Kila hali ili nasi tuweze kutekeleza mpango huu wa kuifanya korosho kuwa zao la kimkakati Wilaya ya Mwanga"alisema Mkwizu .
Akipokea shukrani hizo Mh Diwani wa viti maalumu Blandina Mawala alisema kuwa kwa niaba ya Mh Mwenyekiti wa Halmshaur ya Wilaya ya Manyoni wamefurahishwa sana na umoja huo wa waheshiimiwa hao kutoka Mwanga kuja kutembelea Manyoni lakini pia kuona miradi ambayo inaendelezwa Manyoni na hasa zao la kimkakati la korosho.
Mh Mawala amesema kuwa Halmashaur ya Wilaya ya Manyoni inasimamia kikamilifu kuona kwamba ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kuboresha kilimo inakuwa na tija na inatekelezwa kikamilifu,na hasa katika uboreshaji wa mazao ya kimkakati Kama vile zao la korosho.
Aidha Mh Mawala amewapongeza timu hiyo kwa ujumla na wengine kwa kuona kuwa Kuna tija na haja kuchukua hatua kuja kuwatembelea Manyoni na hawakuona hajaya kuita wataalamu hukohuko kutoka sehemu nyingine na kwamba wameiamini Manyoni kuwa Kwanza inaweza kuwa sehemu ya kuwafungua wao .
"Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashaur na kwa niaba ya Mh Mbunge Dkt Pius Chaya na waheshimiwa Madiwani wote niwapongeze kwa hatua mliyochukua ya kuona Manyoni inafaa kuwa chachu na tija ya nyie kujifunza hivyo niseme mmetuamini Sana nasi tutaendelea kuwa sehemu ya kushirikiana nanyi kwa jinsi ambavyo mmetuamini hatutawaangusha karibuni Tena tena tutakuwa pamoja na hata Sasa mkihitaji Wataalamu kutoka Manyoni kuja Mwanga Basi niseme tu wako tayari watakuja hivyo niwashukuru Sana" alisema Mh Mawala.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.