- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Fadhili Chimsala amethibitisha kupokea Tani 50 za mbegu ya Alizeti tarehe 02 Disemba 2022 ambazo zimehifadhiwa katika ghala la Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Mbegu hizi zitasambazwa katika kila kata ili kuwafikia wanufaika katika eneo husika.
Ndg Chimsala amesema "Kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, wakulima na wananchi kwa ujumla tunaishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Raisi wetu Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuwathamini wakulima na kuhakikisha wanapata pembejeo za kilimo kwa wakati na kwa garama nafuu, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tuliomba tani 50 za mbegu na tumepata zote Tani 50"
Afisa kilimo ndg Zakayo Ijojo alisema;Mbegu hizi za Record C1 ni mbegu bora na imethibitishwa na mamlaka ya udhibiti wa mbegu Tanzania,Aidha tunaishukuru serikali kwa kuleta mbegu hizi zikiwa na garamaa nafuu sana kwani Mbegu hizi zitauzwa kwa shilingi 5,000/= kwa kilo moja na kilo mbili itakua ni 10,000/=.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe Rahabu Mwagisa alisema "Tunaishukuru Serikali yetu kwakuwa sikivu sana kwa wananchi wake , Wilaya yangu imepokea jumla ya Tani 80 za mbegu ya Alizeti kwa maana ya Halmashauri ya Manyoni tani 50 na Halmashauri ya Itigi tani 30 na sisi kwa nafasi zetu tutaendelea kuhamasisha kilimo chenye tija kwenye maeneo yetu lakini pia tutahakikisha mbegu hizi zinawafikia walengwa ambao ni wakulima. Pia Nawaomba wakulima waendelee kuwatumia wataalamu wetu wa kilimo waliopo kwenye maeneo yao ili wawape ushauri juu ya kilimo bora.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.