- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Hekari moja ya shamba la pamba likilimwa kwa kutumia kipimo kipya cha kilimo cha pamba yani sentimita 60 kwa sentimita 30 litakua na miche 44,444 na utavuna kilo 2500.Na kwa sasa Serikali kupitia Wizara ya kilimo imetoa bei elekezi kuwa kilo moja ya pamba iuzwe shilingi 1560.
Haya yamesemwa na Balozi wa pamba Nchini Tanzania Ndg Agrey Mwanri alipokua akitoa Elimu juu ya kilimo hicho cha pamba kwa wakulima na wadau wa kilimo katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Manyoni leo tarehe 10 oktoba 2022.
Wakulima na wadau mbalimbali wakimsikiliza Balozi wa Pamba
Balozi Mwanri Alisema,”Kilimo cha pamba hakihitaji mvua nyingi isipokua wakulima mnapaswa kufata taratibu za namna ya kupanda zao la pamba, kuweka mbolea, kutumia viatilifu na kulitunza zao la pamba kwa kufanya palizi nzuri. Pia nashauri wakulima msipende kutumia mbolea iliyokaa juani kwa muda mrefu kwani jua hupunguza virutubisho kwenye mbolea.
Pamba ilimwe kwa mkakati ili iwe na manufaa na hii itaongeza kipato kwa familia ,mapato kwa Halmashauri lakini pia ni ajira na tukienda mbali Zaidi viwanda vingi vitahuishwa kwani vilifungwa kwa kukosa malighafi hizo. Alisisitiza Balozi Mwanri
Balozi Mwanri pia alisema, "Serikali ya awamu ya sita chini ya Raisi Samia Suluhu Hassani imeamua kuwashika mkono wakulima wadogo wadogo kwa kutoa mbegu, viatilifu na mbolea ya ruzuku ili kuwasaidia wakulima hao kukuza uchumi wao hivyo changamkieni fursa hii wakulima wa Wilaya ya Manyoni".
Nae Afisa Kilimo Halmashauri ya Manyoni Ndg Fadhili Chimsala kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni alisema “Mafunzo haya tumeyaelewa kikamilifu nasi tunakuahidi kuyasimamia ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao la pamba katika halmashauri yetu na msimu tayari umefika nawashauri wakulima wakaandae mashamba kwaajili ya kilimo hiki.
Bi Leila Sawe Muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya alihitimisha kwa kusema , “tunashukuru kwa mbinu nzuri ya Useminishaji naamini wakulima wote na wadau tumeelewa soma lako hivyo maazimio yetu ni Maafisa kilimo wa Halmashauri zote mbili,watendaji wa kata na vijiji pamoja na maafisa ugani waandae kanzi data ya wakulima wetu ili tujue uhitaji wa mbegu na viatilifu pamoja na wahitaji wa majembe ya kulimia
Tutahakikisha wakulima wote wanajua umuhimu wa kilimo hiki cha pamba katika Wilaya ya Manyoni na kuhakikisha wanafata utaratibu mpya wa kilimo hiki cha pamba ili walime kwa manufaa.
Baloza wa pamba akiendelea kutoa elimu juu ya umuhimu na faida za kilimo cha pamba
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.