- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Dkt Vincent Mashinji amefanya kikao na Watumishi wote wa Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni,KU pamoja na Wakuu wa Taasisi zote zilizopo Wilaya ya Manyoni.
Kikao hiki kimefanyika tarehe 12 Agosti 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na Lengo kuu ikiwa ni Kujitambulisha na kufahamiana.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Dkt Mashinji amesema Mambo makuu kadhaa ya Watumishi kuzingatia wakati wa Utendaji kazi kipindi yeye akiwa Mkuu wa Wilaya Manyoni
" Naomba mzingatie yafuatayo kwanza kila mtumishi atambue yeye ni mwakilishi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sehemu yake hivyo anapaswa kumlinda Mhe Rais na kulinda Taswira yake kwa kuwajibika ipasavyo kwenye nafasi yake,
Pili Kukusanya Mapato ni wajibu wa kila mmoja wetu hivyo tujitahidi Kukusanya Mapato na kusimamia ukusanyaji wa mapato"
Sambamba na hilo Dkt Mashinji amewakumbusha Watumishi kuzingatia suala la Lishe maana ni ajenda ya Mhe. Rais kwa kuhakikisha wananchi wanapata Lishe Bora na wanafunzi mashuleni wanapata chakula pindi wanapokua shule.
Vile vile Mhe. Dkt Mashinji amewataka Watumishi wa Wilaya ya Manyoni kusimamia miradi ya Maendeleo vizuri na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na inakua na ubora unaolingana na thamani ya Fedha zinazotolewa na Serikali.
Pia Dkt Mashinji amewataka Watumishi wote kujiendeleza Kielimu kila mmoja alipoishia
" Ninawaomba kila mmoja alipoishia Kielimu ahakikishe anaendelea kusoma usiridhike na Elimu uliyonayo jiendeleze maana Siku hizi unaweza soma hata ukiwa Nyumbani"
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Bi Anastazia Tutuba amemkaribisha Mkuu wa Wilaya Mhe. Dkt Vincent Mashinji kwa niaba ya Watumishi wote
"Kiongozi wetu tunakukaribisha sana Manyoni Tunaahidi kukupa ushirikiano Ili kuijenga Manyoni yetu"
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.