- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Jaji kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Jaji Mustapher Siyani ameyasema haya leo tarehe 30 Januari alipokua kwenye Hafla ya uzinduzi wa Majengo ya Mahakama za Wilaya ya Manyoni, Bunda, Kilindi, Sikonge na Rungwe iliyofanyika kwenye viwanja vya Mahakama mpya ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
“Kuweni mabalozi wazuri wa Haki kwa kuhakikisha mnatoa huduma bora kwa wananchi, jengeni Imani kwa wananchi kwa kuhakikisha mnatoa haki kwa wananchi kwa wakati ili kuepuka dhania ya wananchi kuwa hakuna huduma inatolewa na mahakama bure bila rushwa. Tunao uwezo huo wa kubadili fikra hizo kutoka kwenye kutokuaminiwa kwenda kwenye kuaminiwa kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa haki lakini bila kufanya hivyo tutazidi kunyooshewa vidole kuwa hatutendi haki”.
Jaji Siyani amesema “Ninawaasa watumishi wa Mahakama zote kujivunia na kujisifu kwa kutoa huduma bora kila mmoja kwa nafasi yake na sio kujisifu kwa vitu vingine kama majengo mazuri na mengineyo. Huduma bora ni pamoja na kuhakikisha miundombinu inaboreshwa ndio maana Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Raisi wetu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani imeliona hili ndio maana leo hii tunazindua Mahakama hizi tano (5) zenye miundombinu Mizuri kabisa”
“Serikali imeamua kuboresha upatikanaji wa huduma za Mahakama karibu sana na wananchi ili kuondoa changamoto ya wananchi kufata huduma hii kwa umbali mrefu sana kutoka katika maeneo wanayoishi hivyo tunapaswa kuishukuru serikali yetu ya awamu ya Sita. Huduma zote muhimu za Kisheria zitapatikana katika majengo yetu haya ya Mahakama kama vile Polisi na Ustawi wa Jamii ili kuepusha usumbufu wa huduma za mahakama”. Alisisitiza Jaji Siyani.
Sambamba na hayo kwa zama hizi tunapasw kutambua umuhimu wa matumizi ya Teknolojia katika utoaji wa huduma, Hakuna huduma bora kwa zama hizi bila matumizi ya teknolojia,Kama tulivyoskia wanakwaya wetu wakisema hapa kuwa Mahakanma zetyu zinakwenda kurahisisha huduma zake za kimahakama kwa kutumia teknolojia.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Manyoni.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.