- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
"Jukumu la kulinda miundombinu ya Barabara hii ni letu sote ili kuhakikisha miundombinu yetu inakua salama wakati wote" Haya yamesemwa na SP Ahmed Makele OCD Manyoni akizungumza na wananchi akiwa kata ya Makanda alipokua akikagua na kuona namna wanachi wanavokua chanzo cha uharibifu wa miundombinu hiyo ya barabara ya kintinku- makanda.
SP Makele alisema; Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuhakikisha inaboresha barabara zetu hizi kupitia wakala wa barabara za vijijini yani TARURA ili kuwepo na mawasiliano kati ya kijij na kijij na serikali inatumia fedha nyingi sana lakini badala wananchi tuoneshe kuunga mkono juhudi za Serikali yetu sisi ndio tunakua wa Kwanza kuharibu.
Nitoe wito kwa wananchi wote katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Manyoni kutunza na kulinda Miundombinu na kwa yeyote atakaebainika anafanya uharibifu wa aina yoyote katika miundombinu hii hatua stahiki zitachukuliwa juu yake mara moja kwani hatuko tayari kuona tunakosa mawasiliano kati ya kijij na kijij kwa sababu ya watu wachache wasiopenda maendeleo. Alisisitiza SP Makele.
Nae Engineer wa Tarura Ndg Boniface Ongati alisema; Barabara hii tumeitengeneza kwa garama kubwa ili kuhakikisha tunakua na barabara nzuri ambayo itadumu kwa muda mrefu, Tumejenga kwa kiwango kinachotakiwa sasa basi wananchi lazima tujivunie barabara yetu na kuhakikisaha tunailinda lakini kama tutakuwa waharibifu wa barabara hizi sheria zipo hivyo tutawachukulia sheria wale wote watakaobainika wanaharibu miundombinu ya barabara.
Pia leo tumeleta mashine ambayo itaendelea kutengeneza baadhi ya sehemu ili kuimaririsha barabara hii kuwa imara zaidi hivyo tuendelee kutoa ushirikiano kwa wataalamu wetu ili kuhakikisha tunamaliza marekebisho hayo madogo madogo.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.