- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tarehe 25 Julai 2023 Kamati ya Siasa Mkoa wa Sigida ikiongozwa na Mjumbe wa NEC Ndg. Yohana Msita wametembelea na Kukagua miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Kikundi cha Hope kilichopata Mkopo kutoka Halmashauri, Ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na mabweni Shule ya Sekondari Mwanzi, Ujenzi wa Zahanati ya Mbwasa, Ujenzi wa vyumba viwili vya Awali vya mfano Shule ya Msingi Chikuyu.
Kamati ya Siasa ya Mkoa imepogeza hatua za ujenzi wa miradi hii kwakua miradi hii hatua ni nzuri na imeshauri kuongeza kasi zaidi ili kuhakikisha inakamilika kwa asilimia mia haraka iwezekanavyo.
Ndg. Yohana Msita Mjumbe wa NEC amesema” Nawapongeza kwa hatua hii ya ujenzi kasi ni nzuri hivyo niwaombe kuongeza juhudi zaidi ili kuhakikisha miradi hii kwa sehemu iliyobaki inakamilika kwa wakati na Majengo yanaanza kutumika”.
Tunamshukuru Raisi wa Awamu ya Sita Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kutupatia fedha nyingi za maendeleo katika Mkoa wa Singida hususani hapa Manyoni, tumepata fedha nyingi sana za miradi katika sekta ya Elimu, Afya, Barabara na zinginezo. Amesema Ndg. Msita
Ndg Yohana Msita Amesema; Niwaombe sana Viongozi wenzangu na wataalamu kuendelea kuwashirikisha wananchi katika miradi kwa kushiriki kujitolea katika kazi mbalimbali ili kujua miradi inayoendelea katika maeneo yao na kuunga mkono juhudi za Serikali yetu chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan lakini pia tuitunze miundombinu hii kwa faida ya vizazi vijavyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg. Jimson Mhagama Amesema; Tumepokea Ushauri na Maelekezo yote mliyotupatia tunaahidi kufanyia kazi ili kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa haraka lakini ikiwa na viwango vinavyostahili. Tunawashukuru sana kwa kututembelea na kukagua kuona namna Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tunavyotekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Muonekano wa hatua ya Ujenzi wa Madarasa Shule ya Sekondari Mwanzi.
Muonekano wa Hatua ya Ujenzi Zahanati ya Mbwasa.
Muonekano wa Madarasa ya Awaili ya Mfano Shule ya Msingi Chikuyu.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.