- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
:
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Vincent Mashinji ameongoza kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi - PHC kilichoketi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa J - Max Hotel tarehe 25 Aprili 2025 kwa ajili ya kujadili mikakati ya zoezi la kitaifa la utoaji wa Dozi ya Nyongeza ya Chanjo ya Sindano ya Polio - IPV2 ambalo linatarajiwa kuanza tarehe 1 Mei 2025.
Mhe. Mashinji amewapongeza Wajumbe wa Kamati ya Chanjo ya Halmashauri kwa juhudi na mafanikio makubwa katika kuhakikisha watoto wanapata huduma muhimu za chanjo.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana hadi sasa ni matokeo ya ushirikiano madhubuti kati ya wataalamu wa afya, viongozi dini, viongozi wa jamii na wadau mbalimbali.
Amesisitiza kuwa nyongeza ya dozi ya pili ya chanjo ya polio ya sindano - IPV2 ni hatua muhimu katika kuimarisha kinga kwa watoto dhidi ya ugonjwa hatari wa Polio.
Chanjo ya OPV hutolewa kwa watoto mara tu wanapozaliwa, na kuendelea kutolewa wanapofikisha umri wa wiki 6, 10 na 14. Kwa sasa Chanjo ya IPV hutolewa kwa watoto wakiwa na umri wa wiki 14.
Hivyo, kwa lengo la kuimarisha kinga dhidi ya Ugonjwa wa Polio nchini, watoto wote nchini wataanza kupatiwa dozi ya pili ya Chanjo ya Polio ya IPV2 wanapofikisha miezi 9.
Ili kufanikisha zoezi hilo kwa ufanisi Wajumbe wamekubaliana kuimarisha zaidi uhamasishaji, ufuatiliaji na usimamizi wa utoaji wa chanjo hiyo ili kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa huduma hiyo muhimu.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.