- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wiaya ya Manyoni Mhe Rahabu Mwagisa tarehe 07 Januari 2023 alipokua akizindua kampeni ya upandaji miti iliyofanyika kuzunguka maeneo ya standi ya mabasi Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
“Ninatoa maagizo kwa viongozi wa kata,watendaji na wenyeviti wa vitongoji kuhakikisha kila kaya inapanda miti kuzunguka maeneo yao ya makazi na sambamba na kampeni hii ya upandaji miti niombe pia kuhakikisha usafi unafanyika kila wakati kuzunguka maeneo yetu yote na mazingira yanakuwa safi”.
Mhe. Mwagisa amesema; Tupande miti ili kurekebisha mandhari lakini pia ili kuepusha madhara yatokanayo na ukosekanaji wa miti,madhara ya kukosekana kwa miti hayatokei pale pale madhara yanatoke taratibu hivyo tujitahidi kuzuia madhara hayo kwa kuhakikisha maeneo yote yaliyowazi yanapandwa miti ya kutosha.
Watendaji wa Kata na viongozi wote hakikisheni mnawasisitiza wananchi juu ya kampeni hii pia hakikisheni kwenye barabara zetu na kuzunguka vyanzo vya maji miti inapandwa lakini pia kwenye ofisi zote za Serikali kunakua na miti ya kutosha na itunzwe ili ikue. Alisisitiza Mhe. Mwagisa.
Mimi nashauri Zaidi wananchi kupanda miti ya matunda kwani unapata faida mara mbili yani unapata kivuli lakini pia unapata matunda na unaboresha afya.
MATUKIO KWA PICHA:
Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wakiwa tayari kwa zoezi la upandaji miti.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mhe. Jumanne
Katubu Tawala Wilaya ya Manyoni Ndg. Charles Mkama Adram
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manyoni Ndg. Fadhili Chimsala
ASP Ponsiano Kahongo Akimuwakilisha Kamanda wa Polisi Wilaya
Mshauri wa Jeshi la Akiba Kamanda Enock W. Liwembe.
Mtendaji wa Kata ya Manyoni Ndg. Eiwan Simkonda (kulia) akiwa na mwananchi anaepaswa kutunza mti huu mpaka utakapokua.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.