- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Jumla ya vyumba vya madarasa 16 na matudu ya vyoo 18 vinatarajiwa kujengwa katika maeneo mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya manyoni ili kupunguza upungufu na msongamano wa wanafunzi kupitia mradi mpya wa Boost utakaogarimu Kiasi cha shilingi 909,600,000/=
Akizungumza wakati akifungua kikao cha Kutambulisha mradi huu kwa wajumbe kutoka shule ambazo zimepata bahati ya kutekeleza mradi huu wa Boost Leo tarehe 04 aprili 2023 Afisa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Moleli kwa niaba ya Mkurugenzi amesema,
“Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita chini ya Raisi wake Dkt Samia Suluhu Hasani kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kutuletea mradi huu wa Boost ambao unakwenda kumaliza changamoto ya miundombinu katika sekta ya Elimu kwa kukarabati na kujenga miundombinu ya shule kwa elimu yaa awali na msingi”.
Niwaombe sana wajumbe kila mmoja kwa nafasi yake akatimize majukumu yake na kuhakikisha mradi huu wa Boost unakamilika kwa wakati na unakuwa na ubora unaostahili, Na mradi huu sasa tutakwendas kulipwa kulingana na matokeo yani kama tutamaliza kwa wakati na madarasa yakawa na viwango vinavyohitajika tutakua na firsa ya kuongezewa fedha zingine kwaajili ya kukarabati na kujenga miundombinu mingine kwa shule ambazo bado zina uhitasji lakini kama hatutamaliza kwa waskati maana yake tutaziba fursa ya kuendelea kupata fedha za mradi huu wa Boost. Alisisitiza Ndg Moleli.
Shule ambazo zinakwenda kutekeleza miradi huu kwa awamu ya kwanza ni Shule ya Msingi Chikuyu ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa vya mfano Elimu ya awali Tsh 63,600,000/= , Shule ya msingi Chisingisa ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo vya wanafunzi Tsh 51,100,000/= , Heka ujenzi wa Shule ya msingi mpya Tsh 493,400,000/= ,Shule ya msingi Igwamadete ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na Matundu 3 ya vyoo vya wanafunzi Tsh 74,100,000/= , Ipanduka shule ya msingi ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo vya wanafunzi Tsh 51,100,000/=, Ipululu shule ya msingi ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na Matundu 3 ya vyoo vya wanafunzi Tsh 74,100,000/=, Masigati shule ya msingi ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo vya wanafunzi Tsh 51,100,000/= na Mitoo shule ya msingi ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo vya wanafunzi Tsh 51,100,000/= JUMLA KUU Tsh 909,600,000/=
Naye Afisa Manunuzi Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Charles Mpenzu amesisitiza na kuwaasa wajumbe kuhakikisha wanafata sheria na kanuni za Manunuzi ili kuepusha hoja zinazoweza kujitokeza kwa kutokuzingatia sheria za manunuzi lakini pia amewata wajumbe kuhakikisha matangazo ya zabuni yanatoka na kusambaa sehemu nyingi ili kupata wazabuni wengi na kufanya uchaguzi ulio sahihi kulingana na vigezo vya mzabuni.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.