- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Bi. Leila Sawe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ameongoza kikao cha kujadili na kutoa Maoni ya Dira ya Taifa 2050 kilichofanyika tar 29 Julai 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Akizungumza wakati akifungua kikao hicho Bi. Leila Sawe amesema
" Ni matarajio yangu kuwa tutashiriki vema katika kutoa maoni mazuri kwaajili ya Taifa letu kwa miaka 25 ijayo, Kila mmoja kwa nafasi yake achangie maoni yake"
Kwasasa Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta mbalimbali ikilinganishwa na miaka ya nyuma na hii ni kwasababu miaka 25 iliyopita wapo waliokaa wakaweka mipango ya miaka 25 ambayo inaisha mwakani 2025.Alisema Bi. Leila
Kwa upande wake Bi. Anastazia Tutuba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni amesema Mafanikio katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2025 Nchi yetu imefikia Uchumi wa Kati hivyo tumepiga hatua kubwa sana
" Serikali imechukua hatua madhubuti ya kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo ya Afya, barabara, kuimarisha biashara, usafiri wa maji, usafiri wa anga, Upatikanaji wa Nishati, Elimu na mengine mengi" Alisema.
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni Kielelezo ambacho Taifa linaongozwa nacho kufanikisha matakwa au matumaini ya kuwa na Maisha bora zaidi katika muda uliokusudiwa na matakwa hayo na yakubalike na Taifa husika.
Lengo ni kuchochea kasi ya ukuaji wa Uchumi, kuongeza matumizi ya teknolojia na kuongeza Uzalishaji.
Bi Anastazia Tutuba amesema
"Zoezi hili la Kutoa Maoni ya Dira ya Taifa 2050 limekua ni zoezi shirikishi kwa nchi nzima hivyo washiriki wa Manyoni nao wamepata nafasi hii adhimu ya kuwa sehemu ya kutoa maoni yatakayojumuishwa kwenye uandaaji wa Dira ya 2050 hii ni bahati isiyojirudia kwa wengi hivyo imani yetu ni kuhakikisha uwakilishi wao unakua na maono ya wengi kwa kuiona Tanzania ya miaka 25 ijayo"
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.