- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
''SHULE NANE KWENYE MASHINDANO YA BENDI''
Tarehe 6/12/2023
Ikiwa ni Wiki ya maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara ambayo imeanza tarehe 01 hadi 09 Desemba
Shule 8 za Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ambazo ni Mwembeni Shule ya Msingi, Sayuni Shule ya Msingi, Tambukareli Shule ya Msingi, Majengo Shule ya Msingi, Manyoni Shule ya Msingi, Mwanzi Shule ya Msingi, Mwanzi Sekondari na Mlewa Sekondari.
Zimeshiriki Mashindano ya Kushindanisha Bendi za Shule kwa kuimba Wimbo wa Taifa pamoja na Waafrika Mashariki ambapo wamepatikana washindi katika mashindano hayo ambapo mshindi wa kwanza ni Mwembeni Shule ya Msingi, Mshindi wa pili ni Sayuni Shule ya Msingi na Mshindi wa tatu ni Tambukareli Shule ya Msingi.
Sambamba na mashindano hayo wanafunzi wa Shule zote wamepatiwa Elimu ya kuhifadhi na kujilinda na wanyama pori nane waharibifu kwa Binadamu kutoka kwa Mhifadhi wa Tawa (Tanzania Wildlife Authority) Afisa Wanyamapori Kanda ya Kati Ayubu Sarikiaeli Pallangyo,
Alisema haya "kanda ya kati inasumbuliwa sana na Tembo jinsi ya kupunguza uharibifu wa mnyama huyu pindi unapomwona ni kujua upepo unaelekea wapi na usiruhusu anuse harufu yako, kama upepo unatoka mashariki na kuelekea magharibi na tembo yupo mashariki kaa magharibi napindi unapo mwona unaweza kurudi mita thelathini maana hana uwezo sana wa kuona ivyo hutumia kunusa na kusikia sana,
Na tembo kabla hajakufata huonesha dalili tatu ya kwanza kupanua masikio na kunyanyua mkonge ya pili huanza kurusha mchanga na kuvunja miti kama ipo karibu na ya tatu hubana masikio kuweka mkonge chini na kukufuata, endepo tembo atakufata ameshauri jinsi ya kujiokoa kuna aina mbili ya kwanza kutulia hapohapo ulipo bila kuonesha ishara baya tembo hata kudhuru aina ya pili kuvua nguo uliovaa na kukimbia zigizaga.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.