- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mhe. Kemirembe Lwota Mkuu wa Wilaya ya Manyoni alipokua akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Manyoni Tarehe 12 Julay 2023"
Katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ilikisia kukusanya Jumla ya Tshs 3,186,700,000.00 na kwa kipindi cha Mwezi Julai 2022 hadi Juni 2023 tumekusanya Jumla ya Tshs 2,896,705,409.34 sawa na Asilimia 91 ya makisio ya Makusanyo yote.
Mhe. Kemirembe amesema Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) umejikita katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya,Elimu,Maji safi na salama na sekta zingine hivyo kama serikali tutaendelea kuhakikisha Ilani hii inatekelezwa Ipasavyo kwa kuwapa huduma stahiki wananchi wetu bila kubagua.
Sambamba na hilo Mhe. Kemirembe amewashukuru Viongozi na wananchi wote wa Manyoni kwa kuendelea kutoa ushirikiano kuhakikisha Wilaya ya Manyoni inakua salama.Ninawashuru sana viongozi wetu wa vyama, Dini na wananchi kwa Ujumla kwakutoa ushirikiano kwa vyombo vyetu vya usalama kuhakikisha tunafichua vitendo vya Uhalifu na mpaka sasa Manyoni hali ni nzuri na tunaendelea kuhakikisha Usalama unakuepo kila Wakati
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.