- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mary Kanumba Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Leo tar 14 Disemba 2024 kwenye kikao cha Wenyeviti wa vitongoji na mabalozi wa Kata ya Manyoni pamoja na wadau wa usafi wa Mazingira
"Lazima mji wetu wa Manyoni tuhakikishe unakua safi kwa kuzingatia taratibu zote za usafi lakini ikiwa ni pamoja na kuunga mkono mkakati wa taka zetu kuzolewa na kupelekwa sehemu iliyotengwa ila kuepuka magonjwa ya milipuko"
Naye Swed Seifu Mkuu wa kitengo cha Kudhibiti taka na usafi wa Mazingira amesema ni lazima tuhakikishe tunaweka Mazingira katika hali ya usafi kwa kufuata utaratbu wetu wa kutunza taka sehemu nzuri na hatimae taka hizo kupitiwa na magari na kwa ratiba ambayo mtapewa, Jitihada za kutunza Mazingira na kuyaweka safi ni jukumu letu sote Ili kuepuka magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
Kwa upande wa Kampuni ya JAKAIT INTEGRITY SERVICES ambao ndio wamepata zabuni ya kuzoa taka na kuweka mji wa Manyoni safi Ndg Lameck Ladsilaus Afisa Masoko akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni amesema
" Sisi ni wazoefu sana kwa Kazi hii tumefanya kwenye miji mingi, tunaahidi kushirikiana nayi vizuri Ili kazi yetu iwe rahisi, Tunatoa kipaumbele kwa vijana wenyeji katika kazi hii ili nao pia wapate ajira na kipato kupitia kazi hii ya uzoaji taka"
Diwani Kata ya Manyoni Mhe. Simon Mapunda amewaomba Wenyeviti wa vitongoji na mabalozi kuwapa ushirikiano wa kutosha wadau hawa waliopata zabuni hii na kuhakikisha wanatoa Elimu na taarifa vizuri kwa wananchi Ili kurahisisha zoezi hili la kuweka mji wa Manyoni safi.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.