- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Muwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Bi Mariam Hussein Hassani kwenye kikao cha kawaida cha kisheria cha robo ya kwanza 2022/2023 cha Lishe kilichofanyika tarehe 10 Novemba 2022 ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
Bi Mariamu Hassani alisema suala la Lishe ni suala la muhimu sana hivyo tunapokutana kwenye vikao hivi ni lazima tufanye tathimini ya maazimio yaliyopita na kuona tumefanikiwa kwa kiasi gani lakini pia lazima tukumbushane wajibu wetu kila mmoja kwa nafasi yake juu ya namna gani jamii yetu inaweza kupata Lishe bora.
Watoto wenye Lishe bora wanakua na akili hata maendeleo yao ya kukua na hata maendeleo yao ya shuleni ni tofauti na Watoto ambao hawana lishe bora hivyo kupitia kikao hiki tupate taarifa yetu ya robo iliyopita tuijadili na kisha kuoanga mikakati ya robo ijayo lengo ni kuona tunapiga hatua mbele kumuunga mkono Raisi wa awamu ya sita Mh Samia Suluhu Hassani juu ya mpango huu wa Lishe Kitaifa.Alisisitiza Bi Mariamu Hassani
Kwa upande wake Mganga mkuu Wilaya ya Manyoni Dr Furaha Mwakafwila nae alisema; Tuna kigezo kipya cha mpango huu wa Lishe ambacho ni wanafunzi kupata chakula mashuleni hivyo kwa pamoja kama wajumbe wa kikao hiki tushirikiane kwa pamoja tuhakikishe wanafunzi katika shule zetu zote wanapata lishe bora mashuleni
Dr Mwakafwila alisema; Jamii yetu inaweza kuwa na vyakula vingi sana lakini ikawa haipati lishe bora na hii ni kutokana na jamii kutokujua ni vyakula vipi vinatakiwa kutumika kwa pamoja ili wapate lishe bora hivyo mimi na timu yangu tutaendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi ya vyakula vinavyopatikana katika jamii yetu ambavyo vikitumika jamii yetu itakua inapata Lishe bora.
Leo Tumepata fursa ya kupima afya zetu kama kupima uzito, urefu,presha na mengineyo kwakua tumekuja na huduma hii kwenye kikao hiki. Niwaombe sana tuwe na mazoea ya kupima na kujua Afya zetu mara kwa mara hii itasaidia kujua tatizo mapema kabla tatizo halijawa kubwa sana na kuanza kupata huduma ya matibabu mapema;Alisisitiza Dr Mwakafwila.
wajumbe wa kikao wakiendelea na majadiliano
Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Sambu Nala alisema;Nawashukuru wajumbe wote kwa ushirikiano wenu mlionipa kwa robo hii iliyopita kwani inaonesha wazi namna gani tunathamini Afya za jamii inayotuzunguka. Tumeendelea kusimamia utoaji wa elimu ya ulishaji katika vituo vya kutolea huduma na pia kuwasimamia watoa huduma vituo vyote vya kutolea huduma wanawapima na kuchunguza hali ya lishe ya Watoto na wajawazito kwenye vituo vyao.
Julai mpaka septemba Zaidi ya Wazazi/walezi 32807 wamepata Elimu ya lishe bora kwa Watoto wadogo Miezi 0 -23 na Watoto chini ya miaka mitano 23330 walichunguzwa hali zao za lishe na ambao walionekana na lishe duni walipata ushauri na matibabu mbadala na hali zao za lishe zikaimarika.Hivyo tuendelee kupeana ushirikiano kuhakikisha jamii yetu inapata lishe bora kwa kutumia vyakula vyetu vinavyopatikana katika jamii yetu. Alisema Afisa lishe.
Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.