- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maafisa Ardhi Manyoni Waendelea Kuielimisha Jamii Kuhusu Ulipaji wa Kodi ya Ardhi
Manyoni, 28 Agosti 2025 Katika jitihada za kuhamasisha ulipaji wa kodi na kuongeza uelewa kwa wananchi, Maafisa Ardhi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wameendelea na Ziara ya kutoa elimu na kuwakumbusha wananchi wajibu wao wa kulipia kodi za ardhi.
Ziara hiyo imeongozwa na Afisa Ardhi wa Wilaya, Bw. Mwakila P. Uswege, ambaye aliwafikia wananchi katika Makazi nakutoa Elimu alisema Tunauisha taarifa za site na ofisini, penye matumizi ya makazi waliojenga kuweka biashara wanapewa utaratibu wa kubadilisha matumizi, tunauisha taarifa ili wamiliki wapate bili kupitia namba zao za simu
Akizungumza na wakazi wa Makazi ya Mtaa wa Uarabuni, Bw. Mwakila alieleza kuwa kodi ya ardhi ni ya lazima kwa kila mmiliki wa ardhi, iwe amejenga au bado, na kusisitiza kuwa: "Kodi ya pango ndiyo ile mnayokatwa kila mwezi kupitia umeme (LUKU), lakini kodi ya ardhi inalipwa kila mwaka kwa ardhi unayomiliki – jenga au usijenge, lazima ulipe."
Aliongeza kuwa kwa sasa Serikali imeboresha mifumo na kuwa tayari wameanza kuwaachia wananchi namba zao za TIN kwa ajili ya kulipa kodi hizo moja kwa moja, na kuwataka wale wenye madeni kulipa haraka ili kuepuka adhabu au hatua za kisheria.
Kampeni hiyo imepokelewa kwa hamasa kubwa, huku wananchi wakitoa pongezi kwa maafisa ardhi kwa kuwasogelea moja kwa moja na kutoa elimu ya msingi inayowawezesha kuelewa wajibu wao wa kisheria na kiuchumi.
@wizara_ya_ardhi @maelezonews @singidars @drmashinjivincent @anastaziatutuba
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.