- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maafisa Ardhi Wilaya ya Manyoni Watembelea Nyumba kwa Nyumba Kuwakumbusha Ulipaji wa Kodi ya Ardhi
Manyoni, 20, Agosti 2025 – Maafisa Ardhi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wameanza kampeni ya kutembelea wananchi nyumba kwa nyumba ili kuwakumbusha na kuwaelimisha juu ya wajibu wa kulipa kodi ya ardhi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuongeza mapato ya ndani na kuimarisha usimamizi wa ardhi.
Kampeni hiyo inalenga kuwafikia wakazi wote wa Manyoni kwa njia ya karibu zaidi, huku maafisa hao wakitoa elimu ya moja kwa moja kuhusu umuhimu wa kulipa kodi hiyo kwa wakati, athari za kutolipa, pamoja na haki na wajibu wa mwananchi katika umiliki wa ardhi.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mwakila pendo Uswege Afisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya wananchi kutolipa kodi ya ardhi kwa wakati, jambo linalochelewesha maendeleo ya miradi ya kijamii inayotegemea mapato ya ndani. “Tunaamini njia hii ya moja kwa moja itaongeza uelewa na kuleta matokeo chanya,” aliongeza.
Wananchi wengi wameipokea kampeni hiyo kwa mtazamo chanya, wakieleza kuwa elimu wanayoipata inawasaidia kuelewa umuhimu wa kutimiza wajibu wao wa kisheria na kuchangia maendeleo ya wilaya.
Zoezi hilo litaendelea katika vijiji na mitaa yote ya Halmashauri kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa.
@wizara_ya_ardhi @singidars @anastaziatutuba @drmashinjivincent @ortamisemi @msemajimkuuwaserikali
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.