- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika kuelimisha Wadau wa Sanaa kuhusu Mikopo inayotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Mwl. James Nchembe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni amefungua mafunzo hayo Leo mapema.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa mafunzo hayo Mwl. James Nchembe
amewahusia wasanii juu ya maudhui ya nyimbo za muda mfupi na nyimbo za kudumu, akaomba wasanii wote kwa ujumla watoe maudhui yakuburudisha na kufundisha jamii Ili jamii pamoja na kuburudika basi zipate kuelimika pia kupitia maudhui hayo.
Mafunzo hayo yametolewa na Afisa Utamaduni Mwandamizi Bi. Nyakaho Mahemba ambapo ameeleza kuwa, lengo la utoaji wa mikopo kwa Wadau wa Sanaa Ili kuongeza ubora wa kazi zao zijiendeshe kibiashara na kuwa na ushindani wa Kimataifa.
Pamoja na mambo mengine, ameeleza kuwa mfuko unatoa aina tatu za mikopo ikiwemo mkopo wa kuendesha shughuli za Sanaa, mkopo wa kununua vifaa vya Sanaa, pamoja na mkopo wa kujikimu au dharura.
Aidha, zoezi la utoaji wa mikopo ni la muendelezo ambapo ofisi za Mfuko wa Utamaduni na Sanaa zipo Dar-es-salam maeneo ya Kivukoni kwenye majengo ya Utumishi.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.