- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Makabidhiano ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni yamefanyika tarehe 17 Machi 2023 ambapo Mkurugenzi anayestafu Ndg. Melekizedeck O. Humbe amemkabidhi Mkurugenzi anaekaimu kiti hicho kwa sasa Ndg. Heri A. Kaombwe.
Makabidhiano haya yamefanyika Mbele ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Manyoni Mhe. Jumanne S. Mlagaza pamoja na Wakuu wa Idara na Wakuu wa Vitengo wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ili kila mmoja kufahamu makabidhiano hayo na kupata nasaha kwa pamoja kutoka kwa Mkurugenzi anaekabidhi lakini pia kwa anaekabidhiwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manayoni Mhe. Jumanne S. Mlagaza amesema; "Mkurugenzi anayestafu alikua akifanya kazi na kusimamia kazi zake ili kuleta matokea chanya hivyo namini hata Mkurugenzi unaekabidhiwa kusimamia kiti hichi utafata nyayo hizo na kuhakikisha tunasonga mbele kuleta maendeleo katika Halmashauri yetu ya Wilaya ya Manyoni".
"Nakuomba Mkurugenzi uliekabidhiwa kiti hiki leo kusimamia Watumishi wote kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anawajibika ipasavyo na kwa bidii katika kufanya kazi na kwa kufata sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma" Alisisitiza Mhe. Mlagaza
Ndg Melekizedeck O. Humbe alisema "Ninawashukuru Baraza la Madiwani pamoja na Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa Ushirikiano mkubwa mlionionesha ndani ya mwaka mmoja niliotumikia katika Halmashauri hii, nashukuru sana kwa juhudi mlizozionesha katika kusimamia miradi ya maendeleo tuliyokuwa tunaitekeleza katika Halmashauri, Niwaombe sana Ushirikiano mlionionesha mimi kwa kipindi chote nikiwa Mkurugenzi hapa huo huo muuoneshe kwa Mkurugenzi ninaemkabidhi kiti hichi leo ili kuendelea kushirikiana katika kutekeleza majukumu yetu na kuleta maendeleo katika Halmashauri ya Manyoni.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Heri A. Kaombwe alisema; Niwashukuru sana kwa Kunikaribisha Manyoni ili kushiriki nanyi katika kutumikia Nchi hii ili kuhakikisha tunasonga mbele katika kuleta maendeleo, Ninaahidi kushirikiana nanyi lakini pia kufata nyayo za Mkurugenzi mstafu katika kuhakikisha Halmashauri inasonga mbele.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ;
Halmashauri ya Manyoni.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.