- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Mwagisa tarehe 21 Disemba amekabidhi madarasa 85 katika Shule mbalimbali Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni zikiwemo shule nne za Sekondari ambazo ndio zinakwenda kuanzishwa Januari 2023 (Mkwese,Makutopora Saranda na Muhalala).
Mhe. Rahabu Mwagisa alisema," Nawashukuru wananchi kwa namna mlivoshiriki kikamilifu kuhakikisha tunafanikiwa kukamilisha Madarsa haya 85 katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni lakini pia niwashukuru kwa kujitokeza Leo hapa Muhalala kwenye hafla fupi hii ya makabidhiano ya madarasa haya baada ya kufanya ziara na kukagua madarasa yote yaliyokamilika ujenzi wake.
"Kipekee nampongeza Mhe.Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutujali na kutupatia fedha nyingi katika sekta ya elimu ili kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora katika mazingira bora na sio kwenye sekta ya elimu tuu bali hata sekta zingine kama barabara, Afya ,Maji na zinginezo". Alisisitiza Mhe Mwagisa.
"Pia nashukuru uongozi wa Mkoa ukiongozwa na Mkuu wetu wa Mkoa Mhe. Peter Serukamba kwa usimamizi mzuri na Ufatiliaji wa Miradi hii mpaka leo kukamilika na Pia nashukuru Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwaamasisha wananchi kufanya matoleo na kushiriki kikamilifu kwenye mirada mbalimbali inayokua ikiendelea katika maeneo yao. ,lakini pia natumia nafasi hii kuwashukuru wabunge wa jimbo la Manyoni mashariki na Manyoni magharibi na pia namshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni pamoja na Watendaji wote wa Halmashauri ya Manyoni kwa kuweza kusimamia miradi ya maendeleo nakukamilika"
.Mhe. Mwagisa alisema; Nawaomba wananchi muitunze miundo mbinu hii ya madarasa kwani hii imekuwa bahati kwenu kuweza kupata madarasa haya na shule hizi mpya kwa kata amabazo hazikua na sekondari na ninawaomba na kuwasisitiza wazazi kuwa Watoto wote waliofaulu wazazi hakikisheni mnanawapeleka shule bila shuruti ifikapo tarehe 9/1/2023
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Mhe. Jumanne Makhanda Alisema; " Wito wangu kwenu wananchi wa Manyoni na msisitizo wangu ni kuwa ifikapo januari wazazi wahakikishe Watoto wote waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanafika shule na kuanza masomo ili kujali na kuunga mkono jitihada za Mh. Rais wetu Samia Suluhu Hassani za kutoa fedha nyingi na mwisho kuweza kuondoa maadui watatu (3) ambao ni Umasikini, Ujinga na Maradhi katika nchi yetu hususani katika Wilaya ya Manyoni".
"Tunawapongeza kwa Usimamizi mzuri wa miradi hii kwani tumeona namna mlivotekeleza na kuunga mkono jitihada za Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani nasi kama chama tumeridhishwa na kazi nzuri na kubwa inayofanywa na Serikali na Halmashauri ya Manyoni katika kuwaletea wananchi maendeleo". Alisisitiza Mhe Makhanda.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manyoni Ndg. Fadhili Chimsala alisema; Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa pesa nyingi kwaajili ya mradi wa maendeleo wa madarasa 85 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na pia tunamshukuru kuu wa Wilaya ya Manyoni kwa ushirikiano wake wakuweza kusimamia mradi huo mpaka kukamilika na leo tunakabidhi. Ninawaomba wazazi kuona umuhimu wa mradi huu kwani umesaidia kwa kiasi kikubwa sana kwani Watoto badala ya kutembea umbali mrefu kwenda shule sasa watasoma katika shule za sekondari zinazopatikana katika kata zao hususani zile kata zilizokua hazina shule ya sekondari (mkwese, Muhalala,Saranda na Makutopora) hivyo mnapaswa kuipongeza serikali kwa hilo".
Ndg Chimsala alisisitiza; Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wafike shule na pia hiki ni kipindi cha kuandikisha watoto kwa darasa la awali na la kwanza hivyo Watoto wote wenye sifa za kuanza darasa la kwanza na elimu ya awali waandikishwe. Pia nawakumbusha wananchi kuwa waunge jitihada za serikali kwa angalau kuanzisha maboma ya nyumba za walimu katika shule hizo ilikuipunguzia mzigo serikali na kwa kufanya hivyo mtachochea maendeleo kwa haraka
Mwisho Diwani kata ya Muhalala Mhe. George Fundi alishukuru kwa niaba ya wananchi; "Nashukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mama yetu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani, nawashukuru Mhe Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na watendaji wote wa Halmashauri ya Manyoni kupata shule ya Sekondari Muhalala mnaona nyuso za wananchi hawa zinavyoonesha furaha juu ya hili. Tunawashukuru sana na tunaahidi yale yote mlioshauri na kutaka yafanyike tunakwenda kushirikiana kama viongozi na wananchi kwa ujumla ila tuendelee kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.