- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Manyoni Yaendelea Kusimamia Afua za Lishe, Afya ya Mama na Mtoto Kupitia Kikao Kazi cha Tathmini ya Utekelezaji
Manyoni, 21 Agosti 2025 – Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni imeendesha kikao kazi muhimu cha kujadili utekelezaji wa mkataba wa lishe, tamko la “Jiongeze Tuwavushe Salama”, pamoja na maendeleo ya Mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa (iCHF).
Kikao hicho kilichoongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya, Mwalimu James Mchembe, kilihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka idara za afya, mipango, ustawi wa jamii, elimu na mashirika yanayoshiriki katika kuboresha afya ya jamii. Katibu wa kikao alikuwa Afisa Mipango na Uratibu, Bi. Mery Kanumba.
Katika kikao hicho, ajenda kuu zilijikita katika:
- Tathmini ya Mkataba wa Lishe ngazi ya halmashauri.
- Utekelezaji wa Tamko la “Jiongeze Tuwavushe Salama” linalolenga kuboresha afya ya mama mjamzito, uzazi salama na malezi ya watoto wachanga;
- Uhamasishaji na maendeleo ya Bima ya Afya iliyoboreshwa (iCHF) ikiwa ni mkakati wa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi;
-Taarifa ya utekelezaji wa programu ya M-MAM kwa kipindi husika.
Mwenyekiti wa kikao, Mwalimu Mchembe, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya idara na sekta mbalimbali katika kutekeleza afua za afya, lishe, na ustawi wa jamii. Alihimiza pia ukusanyaji sahihi wa takwimu na ufuatiliaji wa karibu wa viashiria vya mafanikio katika maeneo yote ya utekelezaji.
Bi. Mery Kanumba, kwa upande wake, alieleza kuwa halmashauri inaendelea kuimarisha mikakati ya utekelezaji kwa kushirikisha jamii, viongozi wa vijiji na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha watoto, akina mama, na familia kwa ujumla wananufaika na afua hizi, Pia aliwataka Maafisa kuwaelimisha Wazazi ili wapate uelewa juu ya umhimu wa lishe mashuleni na kupinga ndoa za utotoni.
Washiriki wa kikao walijadiliana kwa kina changamoto, mafanikio na mikakati ya kuboresha utekelezaji wa afua hizo katika robo inayofuata, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu kuhakikisha jamii ya Manyoni inanufaika na huduma bora za afya na lishe.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.