- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Manyoni Yashuhudia Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 64 ya Jeshi la Magereza Tanzania kwa Shamrashamra na Michezo
Manyoni, 23 Agosti 2025 Jeshi la Magereza Tanzania leo limezindua rasmi Maadhimisho ya Miaka 64 tangu kuanzishwa kwake, katika tukio lililofanyika Gereza Manyoni kwa kuambatana na michezo na ushirikiano wa karibu kati ya magereza na jamii.
Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Dkt. Vincent Mashinji, ambaye alipongeza Jeshi la Magereza kwa mchango wake mkubwa katika urekebishaji wa tabia, usalama wa jamii, na maendeleo ya kijamii kupitia ushirikiano wa karibu na wananchi.
Maadhimisho hayo yalianza saa 12:00 asubuhi kwa jogging ya pamoja, iliyojumuisha askari, wananchi na wadau wa maendeleo, kuanzia viwanja vya mpira wa miguu na Baadaye, bonanza la michezo mbalimbali lilifanyika, likiwemo mpira wa miguu, kuvuta kamba, Mbio za Mita Mia, kujaza maji kwa kijiko kwenye glasi, kukimbiza kuku,Kupima Ukimwi, pamoja na Uchagiaji wa Damu Salama kama ishara ya mshikamano na afya kwa wote.
Katika hotuba yake, Mhe. Mashinji alisisitiza umuhimu wa kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi la Magereza na jamii, akisema: “Kauli mbiu ya mwaka huu inatufundisha kuwa urekebishaji wa wahalifu hauishii ndani ya kuta za gereza pekee, bali ni jukumu la jamii nzima kushiriki katika kuwajenga upya.”
Maadhimisho haya yanaendelea kote nchini yakiwa na kauli mbiu: “Miaka 64 ya Jeshi la Magereza Tanzania kwa ushirikiano wa Magereza na Jamii kwa Urekebishaji Wenye Tija.”
Tukio la leo limeacha ujumbe wa mshikamano, nidhamu na matumaini kwa jamii ya Manyoni, huku likitoa fursa ya kuimarisha afya na mahusiano kati ya vyombo vya ulinzi na wananchi.
@magerezatanzania @singidars @halimadendego @drmashinjivincent @anastaziatutuba @tembo_digital_tv
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.