- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Jumla ya miradi 47 inayohusisha sekta mbalimbali, ikiwemo elimu, afya, maji na miundo mbinu ya Barabara, yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 100.2/-, itatembelewa, kukaguliwa, kuwekewa mawe ya Msingi na kuzinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu, mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego, alisema hayo wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru, kitoka kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, katika Kijiji cha Chikuyu, wilayani Manyoni.
Alisema kuwa, miradi hiyo imetekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh. Bilioni 100.2/-, katika halmashauri zote saba, za mkoa wa Singida.
Dendego alizitaja halmashauri hizo kuwa ni Manyoni, Itigi, Ikungi, halmashauri ya wilaya ya Singida, Manispaa ya Singida, Iramba na Mkalama.
"Mwenge wa Uhuru mwaka huu katika mkoa wa Singida, utahusisha miradi 47 yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 100.2/-...serikali kuu imechangia zaidi ya Sh. Bilioni 30/-, sekta binafsi Sh. Bilioni 67/-, halmashauri za Wilaya Sh. Milioni 667/-, wahisani Sh. Bilioni 1.25/- na wananchi zaidi ya Sh. Milioni 287/-," alifafanua Dendego.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Godfrey Mzava, katika makabidhiano hayo, aliagiza wahusika wa miradi yote itakayotembelewa, kukaguliwa, kuwekewa jiwe la Msingi na kufunguliwa, wahakikishe nyaraka na kumbukumbu zote muhimu za miradi husika, zinakuwepo saiti.
"Niwaombe viongozi na wote wanaobusika na miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru, tukute kumbukumbu za nyaraka na vielelezo halisi vyote, zikiwemo halisi na zile za kopi kule kule eneo la saiti...wataalamu wawepo na maelezo ya kina kuhusu mradi husika ," alisema Mzava.
Akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Singida, tayari kuanza mbio zake wilayani Manyoni, mkuu wa wilaya hiyo, Kemilembe Lwota, alisema itakimbizwa kilomita 80.9 na kuhusika kwenye mraidi Saba yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 2.79/-.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni "Uhifadhi wa Mazingira na uchaguzi wa Serikali za Mitaa, huku mkoani Singida ukitarajiwa kuhitimisha mbio zake julai 12, kabla ya siku hiyo kukabidhiwa mkoani Manyara.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.