- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Rahabu Mwagisa amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo kwani jukumu la kuleta maendeleo ni letu sote." Kila mmoja ajue kwamba anapaswa kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuhakikisha tunaleta maendeleo katika Wilaya yetu ya Manyoni" Mh Mwagisa ameyasema haya alipokua akihitimisha ziara yake kwa Kata ya Manyoni tarehe 09 Novemba 2022 katika viwanja vya Ofisi ya Kitongoji Mwanzi, Ziara ambayo lengo lake kuu ni kukagua miradi mbalimbali, kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Manyoni.
Mama yetu Mh Samia Suluhu Hassani Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ametuletea fedha nyingi sana kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Barabara, Maji, Afya, Elimu, Umeme, Kilimo na miradi mingine mingi ili tupate maendeleo katika wilaya yetu hivyo na sisi kwa nafasi zetu tushiriki shughuli mbalimbali ili kuungana na Mama yetu mpendwa Manyoni isonge mbele.Na kushiriki kwetu katika miradi hii ni kujitolea nguvu kazi katika miradi hii lakini pia kulinda na kuitunza miradi pindi inapokamilika ili idumu. Alisisitiza Mh Mwagisa.
Mh Mwagisa alisema; Mnapokua na changamoto naomba mfike katika ofisi yangu msisubiri mpaka mikutano hii ninayofanya, fikeni ili tupate suluhisho la changamoto zilizoko kwenye jamii inayotuzunguka, Siku ya jumatatu mpaka jumatano ninakuepo Manyoni lakini Alhamisi na ijumaa nakuwa Itigi na hii ni kwasababu mnatambua Wilaya ya Manyoni tuna Halmashauri mbili,Hivyo niwaombe sana mfike kwa kuleta changamoto lakini pia Ushauri ili kuleta maendeleo ya Manyoni.
Afisa Tawala Wilaya Bi Leila Sawe akitambulisha Viongozi na Wataalamu mbalimbali walioongozana na Mkuu wa Wilaya.
Mh Mwagisa akizungumza na wananchi katika viwanja vya ofisi ya kitongoji Mwanzi.
Mh Diwani Kata ya Manyoni Mh Mapunda Alimshukuru Mkuu wa Wilaya Alisema; "Kwa niaba ya Madiwani viti maalumu na wananchi wa Kata ya Manyoni kwa ujumla Tunakupongeza na kukushukuru kwa Ziara yako ambayo imeleta matokeo chanya kwa kusikiliza kero zetu na nyingi kuzitatua papo kwa papo lakini zingine zikiendelea kupata ufumbuzi, Kweli kina mama mnaweza.Tunakukaribisha tena na tena na Tunakuahidi yale yote uliyosema tuyasimamie tutayasimamia na kuhakikisha tunashirikiana kwa pamoja ili kuleta maendeleo ya Manyoni kwa pamoja.Nawakaribisha wananchi wote wa manyoni katika ofisi yangu ya Diwani kata ya manyoni ili tuendelee kutatua kero mbalimbali za wananchi lakini pia kwa ushauri .
Viongozi mbalimbali na Wataalamu waliohudhuria mkutano
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya Mh Rahabu Mwagisa
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.