- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota amewataka Viongozi kutoka maeneo mbalimbali wenye miradi ya Boost kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo kikamilifu, kumaliza kwa wakati na miradi kuwa na viwango vinavyostahili kama ilivyoelekezwa kwenye Muongozo wa Ujenzi wa Miradi hiyo.
Mhe. kemirembe ameyasema haya Jana tarehe 02 May 2023 alipotembelea shule zote za msingi zilizopata fedha hizi za Mradi wa Boost yani Shule mpya inayojengwa kata ya Heka, Shule ya Msingi Ipululu,Shule ya Msingi Masigati, Shule ya Msingi Chukuyu na zingine zote zenye mradi wa Boost
“Niwaombe sana viongozi wenzangu na wasimamizi wote wa miradi hii kuhakikisha tunasimamia miradi hii kikamilifu ili ikamilike kwa haraka na ikiwa na ubora unaostahili, Pia tuhamasishe wananchi kushiriki kazi ndogo ndogo za kujitolea ili kuunga mkono juhudi za Raisi wetu Dkt Samia Suluhu Hassani”
Mhe. Kemirembe amesema tunamshukuru Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuletea Miradi mingi katika Wilaya ya Manyoni ikiwemo huu wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule za msingi (Boost), Kwa kutuboreshea miundombinu hii watoto wetu wanakwenda kusoma vizuri na tunaamini ufaulu unakwenda kuongezeka kwa kasi.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.