- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota mgeni rasmi kwenye Hafla ya kufunga mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba yaliyofanyika tarehe 15 Novemba 2023 katika viwanja vya Jumbe Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
“Niwapongeze Wakufunzi kwa kuwapa Mafunzo haya ya Awali ya Jeshi la Akiba lakini niwapongeze wazazi kwa kukubali na kuwaruhusu vijana hawa kujiunga na mafunzo haya yanayokwenda kuwasaidia ninyi kipekee lakini pia kusaidia jamii, lakini vile vile niwashukuru wote kwakuacha shughuli zenu na kuja kushiriki hafla hii ya vijana hawa wanaomaliza mafunzo yao leo hii.”
“Kipekee niwapongeze vijana 85 mnaomaliza mafunzo haya leo hii na Niwaase mkawe walinzi wazuri wa Amani kwa Taifa lenu, mmepewa mafunzo ya kukamata sawa na Askari asie na cheo ili mkasimamie amani na haki katika jamii yetu, Mkatimize wajibu wenu wa kulinda watu na mali zao na msitumie vibaya mamlaka mliyopewa”.Amesisitiza Mhe. Kemirembe
Mhe. Kemirembe amesema “Tushirikiane kwa pamoja ili kuleta Amani ya Manyoni yetu hii sio kazi ya jeshi la Polisi peke yao au Jeshi la Akiba peke yao hili ni jukumu letu sote wananchi wa Manyoni hivyo tushirikiane ili tuweze kuwa salama kwa maendeleo ya Manyoni yetu.”
“Wote tuliopo hapa leo Nawaasa kuwa Mabalozi wazuri kuchukua tahadhari juu ya Magonjwa ya mlipuko kwani katika Mkoa wa Singida imeripotiwa kuwepo kwa ugonnjwa wa kipindupindu, hivyo tuchukue tahadhari kwa kuhakikisha maeneo yetu yanakua safi na kuhakikisha tunanawa mikoni kwa maji tiririka tunapotoka chooni ili kujikinga na Magonjwa haya ya Mlipuko.”
Naye Luteni Kanali Enock Wiliam Liwembe Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Manyoni Amesema; Vijana hawa wanaomaliza leo mafunzo haya ya jeshi la Akiba tumewafunza Utii, tabia njema, Ulinzi kwa taifa lao, Mafunzo ya Mapigano, Bidii kwenye Utendaji kazi, kupiga shabaha, Mafunzo ya majeshi jiran kama Usalama, Polisi, Zima moto na Uhamiaji.
Wanahitimu Askari wa Jeshi la Akiba 85 ikiwa wanawake 22 na wanaume 63 walioanza mafunzo haya tangu tarehe 03 Julay 2023 na yamedumu kwa takribani miezi minne na leo tarehe 15 Novemba wanahitimu wakiwa na ujuzi wa kutosha tayari kulitumikia Taifa lao.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.