- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Melekzedeck O. Humbe Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tarehe 27 septemba 2022 ametembelea kituo cha Afya Nkonko kuona ujenzi wa jengo la x-ray ulipofikia na kuona namna jengo hilo litakavyomaliziwa kwaajili ya kuanza rasmi matumizi
Ujenzi wa jengo la X-ray
Mkurugenzi amempongea Dr Mwakanyamale mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Nkoko na timu yake kwa ukusanyaji wao wa mapato kiasi cha shilingi milioni 1 na laki 5 au Zaidi kwa mwezi, unaozingatia taratibu za kiserikali yani kulipa kwa njia ya mfumo na fedha kuwekwa banki kwa wakati ambapo utaratibu huo unapelekea kudhibiti utoroshaji wa Mapato.
Mkurugenzi amewataka watumishi wake kuwa waadilifu katika kuwahudumia wananchi na kuhakikisha dawa zinakuwepo za kutosha katika kituo kila wakati na vifaa vyote vitumike ili kuepuka vifaa kuharibika kutokana na kukaa muda mrefu bila kufanya kazi.
Chumba cha Upasuaji kituo cha Afya Nkonko
Aidha DMO alikua na haya ya kusema”Nampongeza Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkonko Baraka Chanzi kwani wameshirikiana vema katika kituo hiki kuweka mikakati kuhakikisha wagonjwa wa msamaha wanapata barua kutoka kwenye vijiji vyao maana wao ndio wanawatambua vizuri walengwa wa huduma ya afya kwa msamaha katika jamii.
Mkurugenzi pia amepita katika zahanati ya Mpola,Chikombo,Heka na Chikola na kukagua mazingira ya zahanati hizo pamoja na uwepo wa dawa,Alisema”msicheze na dawa hakikisheni mnatoa dawa kwa usahihi na mjaze kumbukumbu na pia taarifa za vituo na zahanati zitumwe kwa wakati ikiwemo taarifa za uhitaji wa dawa ,sambamba na hili Mkurugenzi alitoa maagizo zahanati na vituo vya afya vizingatie usafi kwani kuna baadhi ya zahanati usafi hauridhishi na atapita wiki ijayo siku ya jumanne tarehe 4 octoba.
Mkurugenzi akikagua stoo ya dawa Zahanati ya Mpola
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.