- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 24 aprili 2024 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Bi Anastazia Tutuba amewaongoza watumishi pamoja na wananchi wa Manyoni kufanya Usafi kuzunguka eneo la Hospitali ya Wilaya pamoja na Standi kuu ya Mabasi ikiwa ni moja ya shughuli katika kuadhimisha Muungano wetu wa Tanganyika na Zanziba (Tanzania)
Akizungumza na wananchi hao baada ya kumaliza Usafi Bi Anastazia Tutuba amesema...
"Ninawashukuru sana kwa kujitokeza kwa wingi kufanya Usafi leo na Usafi ni jukumu letu hivyo tunapaswa kufanya kila wakati ili maeneo yetu yawe safi yavutie lakini pia kujikinga na magonjwa ya milipuko yatokanayo na mazingira kuwa machafu"
Sambamba na Hilo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Standi ya Shimoni Kesho tarehe 25 Aprili 2024 kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Muungano wetu ambapo ifikapo saa3.00 usiku Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Taifa hivyo tutamsikiliza kwa pamoja tukiwa katika viwanja hivyo vya Standi ya Shimoni
"Niwakaribishe sana kesho kwenye viwanja vya Standi ya Shimoni kuanzia saa 9.00 mchana tutakua na kilele cha Maadhimisho ya Muungano tutakua na burudani mbalimbali lakini mijadala ya mada zinazohusu Muungano zitatolewa na badae saa3.00 usiku tutamsikiliza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akihutubia nchi.
Miaka 60 ya Muungano...."Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letu"
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.