- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba amewaongoza viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Manyoni kwenye zoezi la Upandaji miti na utunzaji mazingira lililofanyika kwenye kata zote za Barabara kuu kutoka Singida kwenda Dodoma (Aghondi mpaka Kintinku) tarehe 21 Januari 2023.
RC Serukamba amesema; Tunapanda miti hii ili Kupendezesha mazingira yetu lakini pia kwaajili ya kupata hewa safi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na kukosekana kwa miti katika maeneo yetu. Ombi langu kwenu viongozi wenzangu pamoja na wananchi Tusiishie tuu kupanda miti hiii leo tuendelee kuwa na hulka ya upandaji miti mara kwa mara na Tuitunze miti hii”.
Natoa Wito kwa Wafugaji kutokupitisha Mifugo yao sehemu ambazo tumepanda miti na kuchungisha miti hii, atakaefanya hivyo apigwe faini ya elfu Hamsini (50,000) kila mti na kisha apande miti hiyo aliyochungisha, Viongozi wenzangu naomba mlisimamie hili kwa kuhakikisha mnaweka sheria hizi ndogo na kuzifanyika kazi ili tuhakikishe wananchi wote wanashiriki zoezi hili kikamilifu na miti tuliyopanda inakua vizuri na tunafikia lengo letu tulilojiwekea la kuboresha mazingira yetu.Amesisitiza RC Serukamba.
Sambamba na hilo Rc Serukamba amepiga marufuku vitendo vya wananchi kukakata miti ovyo hali ambayo inahatarisha mazingira yet una kuagiza hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa wananchi watakao kata miti yetu ovyo.
Nae Mkuu Mkuu wa Wilaya ya manyoni Mhe. Rahabu Mwagisa wakati akishukuru baada ya zoezi hili kuhitimishwa alisema; Tunakushukuru Mkuu wetu wa Mkoa kwa kutuongoza katika zoezi hili la Upandaji miti ambalo mpaka sasa Zaidi ya miti laki mbili imepandwa katika maeneo mbalimbali wilayani hapa.Tunaahidi kwa kushirikiana na viongozi wote kuhakikisha zoezi hili linakua endelevu na miti inasimamiwa ili ikue vizuri.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Manyoni
22/01/2023
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.