- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ikiwa wa ni siku ya pili ya muendelezo wa Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Rahabu Mwagisa amefanya mkutano wake wa Hadhara katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwembeni na katika mkutano huo amegawa Hati za Ardhi kwa wananchi waliolipia ardhi zao na kutimiza vigezo vyote vya kumiliki Hati zao.
Mh Rahabu amewataka wananchi wa Manyoni kupata Hati za Ardhi kwani kwasasa zinapatikana kwa urahisi na haichukui muda mrefu kuzipata,lakini pia kuwa na Hati kunapunguza migogoro ya ardhi inayotokea mara kwa mara kwenye jamii inayotuzunguka na kwa kuwa na Hati kuna faida pia ya ardhi hiyo kupanda thamani na kuweza kupata Mikopo kwenye Taasisi za kifedha.
Mh Mwagisa akikabidhi Hati kwa Wananchi
Mh Mwagisa amesikiliza Kero za Wananchi na Kuzitatua papo kwa papo kwakuwa walikuepo Wakuu wa Divisheni zote na Vitengo pamoja na Wakuu wa Taasisi zote zilizopo Manyoni.Mh Mwagisa mwisho alihitimisha kwa kusema wenye changamoto za Ardhi na hawajafika na vielelezo vyao leo basi kesho wafike navyo ofisi ya ardhi Manyoni wapate kutatuliwa changamoto zao lakini pia changamoto nyingi zilizosemwa kuhusu Hospitali yetu ya Wilaya ninaahidi kuzifatilia kwa karibu na nitakaa na watumishi wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na Uongozi wa Chama cha Mapinduzi ili kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa na wananchi mnapata huduma kwa Usahihi.
Wananchi wakimsikiliza Mh Mwagisa wakati akizungumza nao
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.