- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Rahabu Mwagisa Amewataka watumishi wa Afya kuwa waadilifu katika kazi zao na kwa uchache wao basi wafanye kazi kwa bidii, Ameyasema haya tarehe 17 Novemba 2022 alipofanya kikao na watumishi hao katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni kwa madhumuni ya kutatua changamoto zilizopo katika Hospitali hiyo lakini pia kuboresha huduma zinazotolewa hospitalini hapo.
“Hatusemi kuwa watumishi wa Afya hamfanyi kazi kabisa laa hasha, Pamoja na utendaji wenu wa kazi lakini bado tunapokea changamoto kutoka kwa wananchi wetu ndio maana nimeona vema leo kufika hapa nikiwa na Kamati yangu ya Ulinzi na usalama, Muajiri kwa maana ya Mkurugenzi na Msimamizi wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (Mwenyekiti wa CCM wilaya) Nia ni kukaa pamoja na tutatua changamoto hizo na kuboresha huduma za hospitali. Alisema Mh Mwagisa.
Mh Mwagisa alisema; Wananchi wetu wanahitaji kupokelewa vizuri wanapofika kupata huduma (Customer care) pia wanataka wapate huduma mapema na kwa kauli nzuri lakini inapotokea vitu hivyo wananchi hawapati lazima malalamiko yawepo lakini pia kuna baadhi ya watumishi wanaingia kazini kwa muda wanaotaka wao na wengine kukataa kuingia kwa madai kuwa wanadai fedha za Uhamisho, kama taratibu za malipo zinaendelea watumishi mnapaswa kuingia kazini na kutoa huduma kama kawaida.
Watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni wakiskiliza kwa makini kwenye kikao
Mh Mwagisa Alisema;Tupate Uhalisia wa huduma zinazotolewa katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni ili tujue vifaa vinavyokuja katika hospitali yetu je vinawiana na uhitaji wa vifaa hivyo? Lakini pia tupate idadi ya kina mama wanaojifungua katika hospitali yetu kwa wiki moja na kwa mwezi ili kujua namna tunaweza kuhakikisha vifaa vyao vya kujifungulia vinapatikana kila wakati. Na tuendelee kuwaelimisha wananchi ni dawa gani zinapatikana katika hospitali yetu pindi wanapokuja kupata huduma.
Kwa Watumishi wanaokiuka Maadili yao ya Utumishi wachukuliwe hatua maana tukipata wawili wakawa mfano naamini itasaidia sana ili mradi mtu asionewe hii itakua funzo na kwa walinzi wetu ambao wamegeuza geti kuwa sehemu ya biashara kwa kuuzia kina mama wajawazito vifaa kwa garama kubwa kuanzia sasa naagiza kitendo hiko kikome, Waelimisheni kina mama wajawazito wanapokuja cliniki ya mwisho kabla ya kujifungua kuandaa vifaa ambavyo wanapaswa kuja navyo siku ya kujifungua ili waviandae mapema kuepuka garama za kununua vifaa kwa garama ambazo sio za kawaida. Alisisitiza Mh Mwagisa.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Rahabu Mwagisa
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mh Jumanne Mankhanda Alisema;`Hii ni gereji na mnahudumia watu wengi hivyo penye wengi hapakosi changamoto, Namna ya kupokea wateja wetu (Customer care) sio nzuri lazima hilo tuwekane wazi hasa wodi ya wazazi hili nimeliona mwenyewe na ninalikemea ili kuboresha huduma katika hospitali. Lakini pia najua watumishi mpo wachache ila naomba tuwajibike kwa maslahi mapana ya Nchi yetu.
Wanadamu hatujakamilika ila kama watumishi lazima tuwe na nidhamu ya kazi ,tuepuke kutumia vilevi wakati wa kazi lakini pia tuepuke kuomba Rushwa maana tunajua wazi hili ni Kosa kisheria na ni kukiuka maadili ya kazi zetu. Na Zaidi tutunze mali zilizopo katika hospitali yetu na kila mmoja ahakikishe analinda mapato ya hospitali hii ili tuweze kujiendesha wenyewe tukiwa na mapato ya kutosha, hasa Mapato ya X-ray na Utra-sound naomba yasimamiwe sana maana huko ndiko naona mwanya wa kupotea kwa mapato bado upo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya akizungumza kwenye kikao
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Fadhili Chimsala alisema; Nawapongeza watumishi wa divisheni ya Afya kwa kazi nzuri wanayofanya ila nasikitika kwa baadhi yao sio waadilifu na mimi niseme wazi tuu kwa ambao mnakiuka maadili yenu kama watumishi hatua stahiki zitachukuliwa na hili siwezi kulifumbia macho maana nia yetu ni kuhudumia wananchi kwa maslahi mapana ya nchi na sio vinginevyo hivyo kama utashindwa tutakutaka uwapishe wanaoweza kuwatumikia wananchi kwa kufata taratibu na kanuni za utumishi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni akitafakari kwenye kikao.
Kwa Upande wake Mganga mkuu Wilaya ya Manyoni Dr Furaha Mwakafwila alisema: Tunashukuru sana kwa kikao cha leo tumekua wawazi ili tusaidike na tuboreshe huduma za hospitali yetu. Kuna baadhi ya wanachi wanatoa rushwa halafu hawasemi kwa uongozi kwa wale wanaosema hatua zinachukuliwa papo kwa papo, Tumekua tukichukua hatua za kiutumishi na fedha za wagonjwa kurudi na kwa sasa taratibu zingine za kiutumishi zinachukuliwa na Muajiri kwa maana ya Mkurugenzi.
Pia tutaendelea kuelimisha jamii inayotuzunguka ili wajue Sera ya Afya inasemaje ikiwepo wanaostahili kupata msamaha wa matibabu, Kwanza wazee wanaostahili kupata msamaha wa matibabu wanapaswa kuanzia kwenye ofisi za serikali za mitaa wapate barua za kuthibitisha hali zao ili wapate matibabu na kisha ofisi ya ustawi wa jamii watajiridhisha kuona kama anastahili au laaah. Alisisitiza DR Mwakafwila
Kikao kikiendelea Ukumbi wa Ofisi ya DMO Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.