- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh. Rahabu J.Mwagisa amesisitiza suala la lishe kwa kuwa na mikakati ngazi zote za jamii ili kuzuia Utapiamlo na vifo vya mama wajawazito na watoto.Ameyasema haya leo tarehe 01 novemba 2022 alipokua akifungua kikao maalumu cha Mpango wa Lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Maktaba katika halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Mh Mkuu wa Wilaya wakipitia Tathimini ya Lishe kwa kipindi cha Robo iliyopita yani Julai -septemba 2022.
Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja na Watumishi kutoka Vituo vya Afya na Zahanati mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Mh. Mwagisa alisema tunajaza mikataba leo ya Lishe ninawaomba sana mkafanye kazi ya kuhamasisha jamii kupata lishe iliyo bora kwa kutumia vyakula vya kawaida vinavyopatikana katika jamii inayotuzunguka na kwa kufanya hivyo mtakua mmeutendea haki mkataba mnaojaza leo.Na tathimini inayokuja nategemea kuona mabadiliko zaidi ya tathimini ya leo.Vijiji vifanye Maadhimisho ya siku ya Lishe na vijiji viwe na kanuni na taratibu za lishe ili kuwabana wazazi kwenye suala la lishe kwa watoto na wajawazito.
Watendaji wa Kata wakisaini mikataba ya Lishe
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Fadhili Chimsala akiwasisitiza wajumbe wa kikao cha Lishe kuwajibika ili kuleta matokeo chanya ya mpango huu wa Lishe
Afisa Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Bi Felista Ngua Ameshuhudia kusainiwa kwa mikataba hiyo ya Lishe
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.