- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Hadija Missanga
Manyoni- Singida
Haya ameyasema Siku ya Jana Juni 09, 2023 2023 alipokua akifungua mkutano mkuu wa pamoja wa pili 2022/2023 wa Ruwasa Wilaya ya Manyoni.
Ambapo alikuwa na haya
"Katika maeneo mbalimbali nimeona watu wanafanya shughuli za kilimo karibu na vyanzo vya maji bila kufata tartibu wakati wanafahamu vyanzo vya maji vinatakiwa kuachiwa mita 60 kwa pande zote hivyo Maafisa Tarafa naomba mkawambie hao wanaofanya hivyo karibu na vyanzo vyetu vya maji kuondoka mara moja kabla sijachukua hatua zaidi za kisheria"
“Sambamba na hilo niwaombe sana kuendelea kutunza vyanzo vya maji kwa kuhakikisha pia tunapanda miti mingi kuzunguka vyanzo vyetu na kuitunza miti hiyo ili kuhakikisha inakua kwani tutapendezesha Mazingira lakini pia tutakua kumekutunza na kukilinda chanzo kisikauke”.Alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.
Kwa Upande wake
Mhandisi wa Ruwasa, Gabriel Ngongi amesema lengo la mkutano huu ni kuwajengea uwezo wataalamu wetu kufanya maamuzi katika ngazi ya tarafa, kata na kijiji lakini pia kukusanya taarifa muhimu kuhusiana na utoaji wa huduma ya maji pamoja na kupitia taarfa za utoaji wa huduma ya maji katika ngazi ya kijiji kwa ujumla
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.