- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
SHULE BORA ni mradi wa Serikali unaofadhiliwa na UKAID wenye lengo la kukuza na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji mashuleni ili kuboresha Elimu na kuhakikisha watoto wote wa kitanzania wa kike na wa kiume wanapata elimu bora.
Mradi huu unatekelezwa katika Mikoa Tisa(9) Tanzania bara yani Katavi, Rukwa, Dodoma, Singida, Mara, Simiyu, Pwani, Tanga na Kigoma. Mkoa wa Singida Manyoni ni moja ya Halmashauri ambayo mradi huu wa Shule bora unatekelezwa kwenye shule mbalimbali.
Viongozi mbalimbali wa Mradi wa Shule Bora wamefika Wilayani hapo na kuendelea kuutambulisha mradi huu pamoja na kuona maendeleo ya miradi mbalimbali ya serikali inayotekelezwa inayodhaminiwa na Serikali ya Uingereza( UKAID)
Mkuu wa kitengo cha huduma ya jamii ubalozi wa Uingereza Bi Getrude Mapunda alisema; Nawashukuru sana Viongozi wa mahali hapa; Shule, wazazi na jamii kwa ujumla kwa ushirikiano mliouonesha katika kutekeleza mradi huu ambao tuliwapatia fedha ili shule ipate fedha kwaajili ya kuboresha vitu kadha wa kadha shuleni hapa. Serikali ya Uingereza itaendelea kufadhili fedha ili tuboreshe Ufundishaji na kujifunza.
Nimefurahi kusikia mradi wenu ni wa Ng'ombe wanaotumika kulimia mashamba ya shule lakini pia walimu na watu wengine wakihitaji wanalipia na fedha zinaingia kwenye mfuko wa shule na kikubwa zaidi fedha zinazopatikana zinatumika kununua taulo za kike hili ni jambo zuri sana na jema. Tuangalie namna gani watoto wetu wa kike na wa kiume wanafika shuleni kupata elimu bila changamoto yoyote hii itatathimini maendeleo kwenye jamii inayotuzunguka. Alisisitiza Bi Getrude.
Nae Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Hamisi Milowe alisema; Kwa niaba ya Halmashauri na jamii hii inayotuzunguka tunaahidi kusimamia miradi hii ya Serikali kwa udhamini wa Serikali ya Uingereza ili itusaidie kukuza na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji ili watoto wote wa kike na wa kiume katika jamii hii wapate elimu bila changamoto yoyote Lakini pia Tunashukuru kwa kupanda miti ya matunda ambayo itasaidia watoto kupata lishe kipindi wanapokua shuleni.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.