- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tarehe 27 febuari hadi 01 machi 2023 Mradi wa shule bora umetoa mafunzo kwa Maafisa elimu kata, walimu wakuu na mwenyeviti wa kamati za shule mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
Washiriki wamezungumzia namna Mradi wa Shule Bora ulivowasaidia kuleta ukaribu sana kati yao na wazazi hali inayopelekea ushiriki wao kurahisisha shughuli mbalimbali zinazowahitaji wazazi kama suala ya chakula shuleni, Nguvu kazi kwaajili ya kushiriki ujenzi wa Miundombinu na mengineyo.
Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi Ndg. Hamisi Milowe wakati akifungua mafunzo haya amesema; Mafunzo haya ni ya siku tatu na mtakachoelekezwa hapa nendeni mkazidi kukifanyia kazi ili kuleta mabadiliko chanya kwenye shule zetu za msingi katika Halmashauri yetu ya Wilaya ya Manyoni.
Sambamba na hayo Ndg. Milowe amewataka na kuwasisitizia washiriki wa mafunzo kuwa na ushirikaoano wa hali ya juu baina yao na wazazi ili kuleta urahisi katika masuala yote yanayohusu shule mfano mambo ya Lishe shuleni, mahudhurio ya wanafunzi na hata uboreshaji wa miundombinu ya shule.
Naye Mratibu wa Mradi wa Shule Bora Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Bi. Mary katunzi amesema ; Washiriki wote mnapaswa kujua kuwa mmepewa dhamana ya kuhakikisha tunaboresha ufundishaji na ujifunzaji katika shule zote zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ili kuboresha elimu kwa kuhakikisha shule zote watoto wanahudhuria shuleni kila siku na kupata elimu iitakayowasaidia ili kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya Elimu Tanzania.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.