- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mkoa wa Singida Dkt Elipidius Baganda leo Machi 17,2025 amefungua mafunzo ya siku mbili kwa walimu wa masomo ya Kiingereza na Hisabati katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni uliopo wilayani Manyoni
Akizungumza wakati wa hotuba yake Dkt Baganda amesema “ Shule Bora wamekuwa wadau muhimu katika kushirikiana na Serikali kuinua kiwango na ubora wa elimu kwa kutoa mafunzo kwa walimu katika maeneo yetu na tunaona faida yake.
Mwenendo wa ufaulu wa Mkoa wa Singida ni mzuri kwani katika mitihani ya Taifa ya darasa la Saba mwaka 2024 Somo la kingereza shule 25 zilifaulisha kwa Asilimia mia (100%) aidha shule 495 Ufaulu wake ni chini ya Asilimia 50 (50%) na shule 11 hakuna mwanafunzi aliyefaulu na kwa somo la hisabati shule 280 Ufaulu ulikua chini ya Asilimia 50 (50%) na shule moja hakuna mwanafunzi aliyefaulu hivyo hii inadhihirisha umuhimu wa kuendelea kuimarisha mbinu za ufundishaji na kuboresha Mazingira ya kujifunzia
Sambamba na hayo Dkt Baganda amesema
"Pamoja na Mkoa kufanya vizuri katika Mitihani iliyopita tuliona bado tuna jambo la kufanya, tulifanya tathimini, katika tathmini hiyo tulibaini changamoto mbalimbali, moja wapo ni baadhi ya Shule kutokufanya vizuri kwenye masomo ya Kiingereza na Hesabu.Ninawapongeza na kuwashukuru Shule Bora kwa kukubali kutoa mafunzo haya”
Aidha, amewaasa Washiriki wa mafunzo hayo kutumia muda wao kujifunza, kwani anaamini watakapotulia na kufuatilia mafunzo hayo kwa umakini, yatakuwa na tija kwao, Shule walizotoka na Mkoa kwa ujumla.
“Ninawaomba sana washiriki kuhakikisha mnakuwa makini kusikiliza yote mnayoelekezwa na wakufunzi kwani mmekuja hapa kujifunza,kupewa uzoefu.
Kinachotakiwa mseme kweli kwa dhati kabisa.Ukipewa nafasi ya kusema funguka.Hapa tumekuja kama wataalamu wa elimu, tuelekezane. Mwisho wa Siku tupate kitu ambacho tukirudi katika vituo vyetu kitusaidie kuinua Ufaulu na hilo ndilo lengo letu.
Mafunzo haya ni Sehemu ya Utekelezaji wa Shughuli za Kielimu za Mradi wa Shule Bora zinazofadhiliwa na Serikali ya Uingereza (FCDO) kupitia Serikali ya Tanzania kwa Usimamizi wa Shirika la Cambridge Education.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.