- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Lilian Lundo - MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kuipa nguvu Kamati ya Kutathmini Hali ya Uchumi wa Vyombo vya Habari, baada ya kutoa maelekezo wakati wa hafla ya uzinduzi wa minara ya kurusha matangazo kwa masafa ya ardhini (DTT) kuwa kamati hiyo isifanye haraka kutoa taarifa bali ifanye utafiti wa kina na kutoa taarifa iliyokamilika.
Shukrani hizo zimetolewa leo Mei 23, 2023 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa kamati hiyo ambayo aliiunda Januari 24, 2023.
"Serikali inategemea sana matokeo ya kazi itakayofanywa na kamati hii, katika kutengeneza mifumo itakayobadilisha tasnia ya habari. Tasnia ya habari na changamoto zake haziwezi kumalizwa na matamko ya kisiasa, zitamalizwa kwa kutengenezwa mifumo ambayo inatengenezwa kwa tafiti pamoja na kuhusisha mawazo ya watu wengi," amesema Nape.
Ameendelea kusema kuwa, mwanzoni alitoa miezi mitatu akidhani kazi itakuwa ndogo, lakini kazi imekuwa kubwa na kwa ramani waliochora wataalam hata miezi Sita iliyoomba kuongezewa na kamati inaweza ikawa ni michache.
"Baada ya kupata ripoti nimekubaliana nao, tuwape hiyo miezi sita, badala ya ile mitatu ya mwanzo, ili wakamilishe hii kazi ambayo wameshaianza. Wito wangu kwa Wanahabari na Wadau wa Habari ni kutoa ushirikiano kwa kamati ili wakamilishe kazi, na hatimaye kazi ya Uandishi wa Habari iwe na heshima inayostahili," amesema Nape.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Tido Mhando amesema kuwa, baada ya kuwahusisha wataalam wa masuala ya utafiti wa masuala ya habari na uchumi, kamati iliona inahitaji muda zaidi wa kufanya utafiti huo.
"Suala zima la uchumi haliishii tu kwenye mishahara ya wafanyakazi lakini vilevile mambo mengine mengi, mfano namna gani vyombo vya habari vinaweza kuboresha na kupata mafanikio yanayostahili," amesema Tido.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.