- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Bi Leila Sawe kwa niaba ya Mhe. Kemirembe Lwota Mkuu wa Wilaya ya Manyoni kwenye kikao cha Tathimini ya Mkataba wa Lishe cha Wilaya kilichofanyika leo tarehe 13 Julai 2023 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
"Kwa taarifa yetu ya Utekelezaji wa Viashiria ya Mkataba wa lishe kwa kila Kata kwa robo hii kata zote zina alama ya kijana hivyo niwapongeze sana katika kuhakikisha tunasimamia vizuri katika maeneo yetu..Rai yangu kwenu ni kuwasihi kuhakikisha tunasimamia vizuri Mkataba huu wa Lishe ili kuuunga mkono juhudi za Raisi wetu wa awamu ya sita Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani
Naye Bi Adeline Mwanisi Afisa Elimu Sekondari kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya manyoni amewataka Watendaji wa Kata kuendelea kusimamia Shule zote za Msingi na Sekondari kutoa huduma ya chakula mashuleni ili kuwasaidia wanafunzi kuepuka kukaa muda mrefu bila kupata chakula jambo ambalo linawaathiri sana wanafunzi hao."Shule zote za Msingi na Sekondari zitoe chakula shuleni hata kwa kuanza na uji tuu, kaeni vikao na wazazi, wekeni sheria zenu zitakazowaongoza katika kuendesha zoezi hili ili mpaka kikao kijacho kama kuna shule zilikua zimebaki basi nazo zianze kutoa chakula kwaajili ya wanafunzi".
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.