- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kwa awamu inayoendelea kutoka kata ya Makutopora Wilayani Manyoni mpaka Issaka imetangaza ajira 500 kwa wananchi wa vijiji na vitongoji vinavyopitiwa na mradi huo na kigezo kikubwa ni mwananchi kuwa muaminifu, kitambulisho cha NIDA na wadhamini wawili mmoja akiwa ni kiongozi wa serikali(Mtendaji au Mwenyekiti)
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Suleiman Mwenda ameyasema hayo alipokua kwenye mikutano yake kuzitangaza ajira hizo pamoja na kutoa maelekezo ya namna ya kuomba,Mikutano huyo amefanya katika kata ya Makutopora,Saranda,Muhalala na Manyoni mjini tarehe 19 oktoba 2022.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mh Mwenda.
Mh. Mwenda alisema, “Raisi wa awamu ya sita Mh. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi sana katika Wilaya yetu ya Manyoni ikiwemo TSh Bilioni 20 kwaajili ya ujenzi wa bwawa kubwa la maji(Mbwasa) litakalohudumia miradi minne ya umwagiliaji,Bilioni 1.7 kwaajili ya ujenzi wa madarasa ya sekondari, mradi huu wa Reli ya mwendo kasi unaopita kwetu na miradi mingine mingi,hivyo tunaona namna gani Mh. Raisi anatupenda na kutujali wananchi wa Manyoni”.
Malalamiko yalifikishwa na Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Mh Dkt Pius Chaya kuwa wananchi wake wa vijiji na vitongoji vinavyopitiwa na mradi wa SGR wanakosa Ajira, hivyo kama serikali tukalichukua nakuliwekea muongozo ili mradi uwanufaishe wenyeji wa eneo husika kwa kuwapa wananchi ajira ndio maana leo Mkuu wenu wa wilaya nipo hapa kuwatangazia ajira hizi ambazo pia zitakua chanzo cha maendeleo ya mtu mmoja mmoja kama mtaitumia vizuri.Alisema Mh. Mwenda.
Mh Diwani wa Makutopora akitoa Shukrani kwa niaba ya wananchi wa Makutopora
Mh Mwenda akizungumza na wananchi
Miradi ya Serikali ifanywe kwa uaminifu ili iwe na manufaa kwa jamii na viongozi ninawaomba msimamie tupate watu wenye nguvu,waaminifu na wazalendo watakaofanya hii kazi vizuri ili kuepuka ubadhilifu unaoweza kufanywa na watu kwa kutokua waaminifu mwisho wa siku mradi unajengwa chini ya kiwango.Alisisitiza Mh. Mwenda
Kwa niaba ya wananchi Waheshimiwa madiwani wa Kata za Manyoni,saranda,makutopora na Muhalala waliishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mradi huu ambao utanufaisha wananchi wetu na tunaahidi kwa kushirikiana na watendaji wetu na wenyeviti kusimamia zoezi zima la kupata watu watakaofanya kazi hizo kwa uaminifu na kuusimamia mradi kipindi chote mpaka utakapokamilika.
Viongozi mbalimbali kwenye mkutano akiwemo Mh Diwani kata ya manyoni
Wananchi pia walishukuru kwa fursa wanazoenda kupata kupitia mradi wa SGR
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.