- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serukamba amesema, Mkoa wa Singida ni nusu jangwa na mvua tunayopata inatokana na misitu michache iliyopo katika Mkoa wetu, tukikata misitu yote na Mapori , Singida tutakosa Mvua na hatimaye tutakosa Chakula.
Mheshimiwa Serukamba amesema hayo wakati akiongea na wananchi wa Kijiji cha Msemembo Wilayani Manyoni walipotoa Kero ya TFS kuwazuia Wananchi kufanya Shughuli katika eneo la Msitu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni alisema Wananchi walikaa na Wananchi na kukubaliana kutenge eneo na kulikabidhi eneo hilo kwa TFS ili liweze kusimamiwa na sasa Wananchi wanalitaka eneo hilo kwa ajili ya Shughuli ya Kilimo na ufugaji ambapo ni kinyume na Makabidhiano yaliyofanywa kati ya TFS , Uongozi wa Kijiji na Wananchi.
Aidha Mkuu wa Mkoa amezitaka mamalaka zote zinazosimia maeneo tengefu ya Misitu na Mapori kuendelea kuyalinda ili Vizazi vijavyo waweze kufaidi Matunda ya Uhifadhi wa Misitu Nchini.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Joseph Serukamba ameendelea na ziara Wilaya ya Manyoni kusikiliza na Kutatua Kero za Wananchi na Kukagua Miradi ya Maendeleo.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.